Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 30, 2016

CRISTIANO RONALDO AIPA KOMBE REAL KWA MIKWAJU YA PENATI 5-3.

Wachezaji wa Real Madrid walipozi na wanao kupata picha ya pamoja mara baada ya kupata ushindiNdani ya Uwanja maarufu wa San Siro Jijini Milan, Klabu za Jijini Madrid, Spain ambazo ni Mahasimu, Atlètico Madrid na Real Madrid, zilipambana kwenye Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, na Real kubeba Kombe baada ya kushinda kwa Mikwaju ya Penati 5-3 kufuatia Sare ya 1-1 baada ya Dakika 120 za mchezo.

Timu hizi zilikuwa Sare 1-1 baada ya Dakika 90 na zikaongezwa Dakika za Nyongeza 30 na Matokeo yakabaki hay ohayo na ndipo Penati Tano Tano zikapigwa na Real kuibuka kidedea.
Bao la Real lilifungwa Dakika ya 15 na Atletico kukosa nafasi ya kusawazisha katika Dakika ya 48 baada ya Antoine Griezmann kukosa Penati lakini Dakika ya 79 Yannick Carrasco, alietokea Benchi akasawazisha.
Kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano, Cristiano Ronaldo ndie alieifungia Real Penati ya ushindi baada ya Juanfran kukosa Penati ya Atletico.
Kabla, Lucas Vazquez, Marcelo na Gareth Bale waliifungia Real, huku Atletico wakifunga kupitia Griezmann, Gabi na Saul Niguez na Penati kuwa 3-3.

Sergio Ramos akaipa Real Bao na kuwafanya wawe mbele kwa Penati ya 4-3 lakini Juanfran wa Atletico akapiga Posti na Ronaldo kuja na kufunga Penati ya Tano na kushinda kwa Penati 5-3.
Hii ni mara ya 11 kwa Real Madrid kutwaa Kombe la Ulaya na safari hii wametwaa chini ya Kocha Mkuu Lejendari Zinedine Zidane.
Yannick Ferreira CarrascoDakika 120 zilikatika kwa 1-1 na mikwaju ya penatikupigwaDakika 90 zilikamilika kwa sare ya 1-1 na mtanange kwenda dakika 120Yannick Carrasco of Atletico Madrid celebrates after scoring the equalising goal Yannick CarrascoYannick Carrasco of Atletico Madrid celebrates with a member of the crowd Yannick Ferreira-Carrasco (79') aliisawazishia bao na kufanya 1-1.Dakika ya 47 kipindi cha pili Atletico walikosa mkwaju wa penati uliopigwa na Antoine Griezmann na kugonga mwamba wa juu Ramos dakika ya 15VIKOSI:
Real Madrid XI :
Navas; Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo; Casemiro, Kroos, Modric; Bale, Ronaldo, Benzema
Akiba: Casilla, Nacho, James, Vazquez, Jese, Isco, Danilo
Atletico Madrid XI: Oblak; Juanfran, Savic, Godin, Filipe Luis; Saul, Gabi, Fernandez, Koke; Griezmann, Torres 

RonaldoRobert Pires, Ludovic Giuly na Marcel Desailly ndio watakao shika kipaza sauti kukuletea matangazo moja kwa moja kutoka Uwanjani usiku huu.
SAFARI YA ATLETICO MADRID KUELEKEA HAPA FAINALI:
Galatasaray 0-2 Atletico (group stage)
Atletico 1-2 Benfica (group stage)
Atletico 4-0 Astana (group stage)
Astana 0-0 Atletico (group stage)
Atletico 2-0 Galatasaray (group stage)
Benfica 1-2 Atletico (group stage)
PSV 0-0 Atletico (last 16)
Atletico 0-0 PSV - 8-7 pens (last 16)
Barcelona 2-1 Atletico (quarter-final)
Atletico 2-0 Barcelona (quarter-final)
Atletico 1-0 Bayern Munich (semi-final)
Bayern Munich 2-1 Atletico (semi-final) 


SAFARI YA REAL MADRID KUELEKEA HAPA FAINALI:
Real Madrid 4-0 Shakhtar (group stage)
Malmo 0-2 Real Madrid (group stage)
PSG 0-0 Real Madrid (group stage)
Real Madrid 1-0 PSG (group stage)
Shakhtar 3-4 Real Madrid (group stage)
Real Madrid 8-0 Malmo (group stage)
Roma 0-2 Real Madrid (last 16)
Real Madrid 2-0 Roma (last 16)
Wolfsburg 2-0 Real Madrid (quarter-final)
Real Madrid 3-0 Wolfsburg (quarter-final)
Manchester City 0-0 Real Madrid (semi-final) 

Real Madrid 1-0 Manchester City (semi-final)Mwamuzi wa kipute hikileo ni Fundi umeme Mstahafu, Mark Clattenburg wa England na hapa akiwa tayari kwenye Uwanja wa San Siro.

No comments:

Post a Comment