Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, July 5, 2015

WENYEJI CHILE MABINGWA COPA AMERICA 2015, WAIFUNGA ARGENTINA KWA MIKWAJU YA PENATI PENATI 4-1



Wenyeji Chile wametwaa Taji lao la kwanza kabisa baada ya kuibwaga Argentina kwa Penati 4-1 kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 120 za Fainali ya Copa America, Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, iliyochezwa mbele ya Halaiki ya Mashabiki ndani ya Estadio Nacional Santiago Jijini Santiago. Kipigo hiki kimeendeleza ukame wa Argentina wa Miaka 22 wa kutotwaa Taji lolote tangu walipobeba Copa America Mwaka 1993 huko Ecuador na pia unamfanya Kepteni wao Lionel Messi, aliewahi kuwa Mchezaji Bora Duniani mara 4, aendelee kutokuwa na mafanikio yeyote na Le Albiceleste tofauti na akiwa na Klabu yake FC Barcelona ya Spain. 
Kwa Chile, ushindi huu umemaliza Karne yao ya kushiriki Mashindano bila Taji lolote baada ya kufanikiwa kufika Fainali 4 za Copa America, zile za 1955, 1956, 1979 na 1987, na kufungwa zote.
Chile, chini ya Kocha toka Argentina Jorge Sampaoli, hawakucheza Soka la kuvutia na walikosa nafasi moja ya wazi katika Dakika za Nyongeza 30 wakati Argentina, chini ya Kocha Gerardo 'Tata' Martino, nao walikosa nafasi ya wazi wakati Gonzalo Higuain alipokosa ndani ya Dakika 90.Ushindi! 4-1 kwa mikwaju ya penatiBalaa!! Alexis Sanchez alipowafungia mkwaju wa UshindiAlexis Sanchez akishangilia baada ya kuitoa ArgentinaMikwaju ya penati ikiendelea..Kipa wa Chile Claudio bravo akiwa amebeba juu zawadi yake ya Golden  Grove Eduardo Vargas akiwa na mwanae pamoja na Tuzo yakeTASWIRADakika 120 zilimalizika bila kufungana tena kwa kutoka 0-0 na mikwaju ya penati kupigwa!Dakika 90 zilimalizika bila kufungana na kuongezwa muda wa dakika 30!Angel Di Maria akubali yaishe mapema kipindi cha kwanza! Lavezzi alichukuwa nafasi yakeKipindi cha pili kinaendelea..Mashabiki wenyeji chile!VIKOSI:
Argentina Wanaoanza:
Romero, Zabaleta, Demichelis, Otamendi, Rojo, Biglia, Mascherano, Pastore, Messi, Aguero, Di Maria
Chile wanaoanza: Bravo, Isla, Medel, Silva, Beausejour, Aranguiz, Diaz, Vidal, Valdivia, Sanchez, Vargas


No comments:

Post a Comment