Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 18, 2014

MAN CITY YAANZA VEMA KUTETEA UBINGWA KWA KUICHAPA NEWCASTLE 2-0

 

Dakika za Majeruhi Sergio Agüero aliwafungia bao safi Man City na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Wenyeji Newcastle United.Silva akishangilia bao lake dhidi ya Newcastle katika dakika ya 38.
BAO za Dakika ya 38 na 90 zimewapa ushindi Mabingwa Manchester City walipocheza Ugenini na Newcastle huko Saint James Park katika Mechi yao ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England Msimu mpya wa 2014/15.
David Silva ndie aliefunga Bao la Kwanza baada ya kutengenezewa vizuri na Edin Dzeko na la Pili kupachikwa katika Dakika za Majeruhi na Sergio Aguero alieingizwa Dakika ya 83 kumbadili Edin Dzeko.
Mechi inayofuata kwa Man City kwenye Ligi ni ya Nyumbani Uwanjani Etihad hapo Jumatatu Agosti 25 watakapowavaa Liverpool.
Taswira kabla ya mtanange kuanza kati ya Newcastle na CityMike Williamson challenges Stevan Jovetic Mike akimkaba Jovetic  Emmanuel Riviere is challenged by Yaya Toure Emmanuel akikabwa kwa sana na Yaya ToureStevan Jovetic controls the ball as Fabricio Coloccini closes in.Jovetic akimiliki mpiraMoussa Sissoko challenges Samir NasriSamir Nasri akilindwa Sergio Aguero scoresAguero akimaliza Mchezo katika dakika za MajeruhiSergio Aguero celebrates after scoring the second goal Usimwambie Mtu!!!
VIKOSI:
Newcastle:
 Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Colback, Anita, Sissoko, Cabella, Gouffran, Riviere.
Subs: Aarons, Perez, Haidara, Elliot, Obertan, Steven Taylor, Abeid.

Manchester City: Hart, Clichy, Demichelis, Kompany, Kolarov, Fernando, Toure, Nasri, Jovetic, Silva, Dzeko.
Subs: Zabaleta, Milner, Caballero, Jesus Navas, Aguero, Fernandinho, Boyata.
Referee: Martin Atkinson 

Shabiki wa timu ya Newcastle akiwa tayari kuucheki mtanange wa Timu hiyo na ikiwa ni mechi yao ya kwanza kwa Msimu huu mpya wa 2014/15

No comments:

Post a Comment