Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 21, 2014

AZAM FC YATUPWA NJE YALAZWA KWA PENATI 4-3 NA EL MARREIKH YA SUDAN KWENYE KAGAME CUP 2014:

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Azam FC ya Chamanzi jijini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kucharazwa mikwaju 4-3 dhidi ya El Marreikh ya Sudani katika mchezo wa pili wa robo fainali.
Wachezaji ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda ndio walioigharimu Azam FC licha ya mlinda mlango Mwadin Ally kufanya kazi nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao.
Wachezaji walioipa tiketi ya kurejea nyumbani Azam FC kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga SC ni beki Shomary Kapombe na mshambuliaji Lionel Saint- Preux kutoka Haiti.

Aidha kocha wa mabingwa hao wapya wa soka la Tanzania, Mcameroon Joseph Marious Omog ameonekana amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mno kuelekea mchezo huo, ambapo mbali na mambo mengine aliwaelekeza mifumo na aina tofauti ya uchezaji, ikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.


Omong aliwaandaa wachezaji wake pia kwa kupiga penalti, lakini hakuna kilichofua dafu kutokana na upigaji wa kimakosa uliofanywa na Kapombe aliyepaisha penati yake juu na gonga mwamba na Preux aliyepiga mpira mwepesi na kumwezesha mlinda mlango wa Merreikh kuificha bila shaka

No comments:

Post a Comment