Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 21, 2014

SIMBA NA YANGA KUMALIZA UBISHI WA MAKOCHA OCTOBA 12, RATIBA LIGI KUU HADHARANI

TFF jana imetoa Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa Msimu mpya wa 2014/15 na Mechi za kwanza kuchezwa Jumamosi Septemba 20.
Ratiba hiyo, iliyosambazwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura, imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, Usajili wa Dirisha Dogo kati ya Novemba 15 na Desemba 15, ushiriki wa Klabu za Azam FC na Yanga kwenye Mashindano ya CAF ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).
Kwa mujibu wa Wambura, mechi zitachezwa Wikiendi tu ili kuongeza msisimko na kuwapa fursa Washabiki wengi zaidi kuhudhuria na katikati ya Wiki kuachwa wazi kwa ajili ya Mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
Vilevile kutakuwa na Mechi kwenye Boxing Day na Siku ya Mwaka Mpya.
Ile Dabi inayongojewa kwa hamu Nchi nzima, Dabi ya Kariakoo, kati ya Yanga na Simba, itachezwa Oktoba 12 na Marudiano ni Februari 8.
Ligi itamalizika rasmi Tarehe 18 Aprili 2015. 



LIGI KUU VODACOM
RATIBA-Mechi za Ufunguzi

Septemba 20
Azam FC v Polisi Moro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Yanga [Jamhuri, Morogoro]
Stand United v Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga]
Mgambo JKT v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandizi]
Mbeya City v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]

Septemba 21
Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

No comments:

Post a Comment