Lazar Markovic |
Hatimaye
Lazar Markovic amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Liverpool kwa
ada ya pauni milioni £19.8 akitokea Benfica na kutuma ujumbe kwa
mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alikuwepo Merseyside
hapo jana kumalizia mambo kadhaa ikiwemo mambo binafsi ametupia katika
ukurasa wake huo ujumbe ambao umeonyesha wazi kuwa hatarejea tena
Estadio da Luz msimu ujao.
‘Ahsante
kwa kila kitu na kwaherini!’ huo ni ujumbe ambao ameutuma asubuhi ya
leo ambao uliambatana na picha yake akiwapungia mashabiki.
Anakuwa
ni mchezaji wa nne wa kiwango cha juu kusajiliwa na Liverpool kiangazi
hii akitanguliwa na Rickie Lambert, Adam Lallana na Emre Can.
No comments:
Post a Comment