Hakuna kitu kizuri zaidi ya nchi yako kushinda kombe la dunia lakini kwa mwanamuziki mzaliwa wa Barbados
Saint Michael, Barbados Rihanna ushindi wa Ujerumani dhidi ya
Argentina ilikuwa ni zaidi ya furaha. Malkia huyo muziki wa Pop duniani
alikuwa akipiga picha kadhaa kuonyesha uwepo wake ndani ya uwanja wa
Maracana usiku wa Jumapili akionekana akishangilia ushindi wa Ujerumani
wa goli 1-0 la dakika 30 za nyongeza.
Nyota huyo wa muziki aliweka picha akionyesha jezi ya timu ya taifa ya Ujerumani kudhihirisha mahaba yake jukwani
Ushangiliaji: Rihanna akifurahia bao 1-0 la dakika za ziada Usiku wa Jumapili.
Naked
chef: Nyota na mwanamitindo na mtaalamu wa mambo ya vyakula wa
Uingereza Jamie Oliver akipiga picha ya kumbukumbu na malkia wa muziki
wa Pop Rihanna ndani ya dimba la Maracana
Mapema kabla ya mchezo Rihanna aliweka picha mtandaoni akiwa na nguli wa soka duniani Edson Arantes do Nascimento Pele ukiwa ni muda mfupi tu akiwa ametua nchini Brazil kuelekea kwenye mchezo wa fainali.
Rihanna
alionekana mwenye furaha na kujisikia faraja kukutana na mtu mashuhuri
'the great Pele'
ambapo nyota huyo wa zamani wa soka wa klabu ya Santos na mshambuliaji
wa zamani wa New York Cosmos pia na kufurahia huku akipiga picha
mfululizo na Rihanna ambazo zilikuwa zinamiminika kupitia ukurasa wake
wa mtandao Twitter.
Brazil, Colombia na Ujerumani ni mataifa ambayo Rihanna alikuwa akiyaunga mkono katika fainali hizo kwa wiki kadhaa zilizopita.
Alikuwa
pia akimpenda sana James Rodriguez, ambaye amechomoza kama mmoja wa
nyota wa kombe la dunia licha ya Colombia kuondolewa mapema katika
fainali hizo.
Rihanna akiwa na nguli wa soka wa dunia Pele
Rihanna akimkumbatia 'The Legendary' Pele baada ya kuwasili Brazil
Rihanna alituma ujumbe wa kuwaunga mkono wenyeji wa fainali Brazil
Rihanna alio0nekana kuvutiwa na James Rodriguez
No comments:
Post a Comment