Lionel
Messi amejikuta katika wakati mwingine mgumu baada ya kumalizika kwa
fainali za kombe la dunia hususani hapo jana kufuatia nguli mwingine wa
sona duniania mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego
Maradona na Bosi mkubwa kabisa wa soka duniani Sepp Blatter kushangazwa
na tuzo na tuzo yake ya mchezaji aliyevutia kwenye kombe la dunia.
Messi
alionekana hakuwa na lolote alilolifanya kulinganisha na wachezaji
wengine baada ya Argentina kufungwa na Ujerumani bao 1-0 katika dakika
za nyongeza uwanja wa Maracana, na kisha kuzawadiwa tuzo ya Golden Ball.
Mshituko
umekuja huku ikidhaniwa pengine walikuwepo wengi waliong'ara zaidi
nyuma yake akiwemo winga wa Uholanzi Arjen Robben au mfungaji wa
michuano hiyo kutoka Colombia James Rodriguez aliyefunga magoli sita
ambaye licha ya kushinda tuzo ya Golden Boot pengine angestahili pia
Golden Ball ambaye kimsingi Maradona ameonekana kumkubali sana.
Ilikuwa
ni timu ya watu wa kiufundi ya FIFA ambayo ilimchagua Messi ambapo
baadaye ikaonekana pengine msuli wa kiushindani wa kibiashara ulitumika
kwa watengenezajiwa wa vifaa vya michezo vya Adidas ambao walidhamini
tuzo ya mshindi wa Golden
Ball ambapo waliamtaka Messi kwa kuwa ni sura ya dunia katika
kuitambulisha bidhaa yao.
No comments:
Post a Comment