Ujerumani
ilimaliza kiu yao ya kusubiri kwa miaka 24 kutwaa kombe la dunia usiku
wa Jumapili ambapo wachezaji walikesha kwa furaha kwa kufikia mafanikio
hayo.
Goli
pekee la Mario
Gotze katika muda wa dakika 30 za nyongeza lilipelekea Ujerumani
kushinda taji lake la nne na kwa mara ya kwanza kama taifa moja kufuatia
kuwachapa Argentina 1-0 uwanja wa Maracana.
Joachim
Low na wachezaji wake walikesha wakisheherekea taji hilo jijini Rio de
Janeiro baada ya mchezo ambapo waliungana na familia zao na wapenzi wao.
Katika
hali isiyotarajiwa mwanamuziki nguli wa kike wa muziki wa Pop Rihanna
aliungana nao ambapo alitumia nafasi hiyo kupiga picha na hata kubusiana
na wachezaji wa timu hiyo ya taifa.
|
Kansela wa UJerumani Angela Markel akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu yake ya Taifa baada ya mchezo. |
|
Rihanna akiwa na Mario Gotdze muuaji wa Argentina kwenye pati |
|
Malkia wa muziki wa Pop Rihanna akipiga picha na mvunja rekodi ya ufungaji kombe la dunia Miroslav Klose |
|
Mtu
kati: Rihanna akishikilia kombe la dunia akiwa katikati ya wapenzi wake
wa muda nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani Podolski na Schweinsteiger
ambao wamempa kiss la nguvu mashavu yote. |
|
Muda wa kusheherekea: Schweinsteiger akiwa na jezi iliyosainiwa akiwa pamoja na mpenzi wake Sarah Brandner ndani ya pati |
|
Ni
tabasamu mwanzo mwisho: Mkurugenzi wa Daimler Dieter Zetsche, kocha
mkuu wa Ujerumani Joachim Low na Rais wa IOC Thomas Bach katika picha ya
pamoja |
No comments:
Post a Comment