Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 14, 2014

LIVERPOOL 3 vs MANCHESTER CITY 2, UBINGWA WANUKIA KWA MAJOGOO LIVERPOOL BAADA YA KUIFUNGA CITY NAKUPAA KILELENI!

Majogoo wa Jiji, Liverpool  Leo wameweka  matumaini yao ya kutwaa Ubingwa wao wa kwanza wa England tangu 1990 na kuacha hatima yao ibakie mikononi mwao wenyewe baada ya kuwachapa Man City, wanaopigania nao Ubingwa, Bao 3-2 katika Mechi iliyochezwa Anfield.
Lakini bado kidogo waukose ushindi huu muhimu kwani waliongoza 2-0 hadi Mapumziko na City kujitutumua Kipindi cha Pili na kusawazisha na Gemu kuwa 2-2 na ndipo ikaja zawadi kwa Liverpool kutoka kwa Nahodha wa City, Vincent Kompany, ambae aliokoa fyongo na Mpira ukamkuta Phillippe Coutinho alieachia Shuti tamu na kuwapa Bao la ushindi.
Man City walipata pigo kwenye Dakika ya 19 wakati Kiungo wao mahiri, Yaya Toure, alipolazimika kutoka baada ya kuumia Goti na nafasi yake kuchukuliwa na Garcia.

Dakika ya 93 Kiungo wa Liverpool Henderson alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mark Clattenburg kwa Rafu mbaya aliyomfanyia Samir Nasri.

Ushindi huu umewabakiza Liverpool kileleni wakiwa na Pointi 77 kwa Mechi 34 wakifuatiwa na Chelsea, ambao watacheza baadae Leo, wakiwa na Pointi 72 kwa Mechi 33 na City kukamata Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 70 kwa Mechi 32.
Asante Baba!!!Mpaka kwa Camera Man!!!Suarez akiendesha...Yaya Toure ....hoi!!! katika dakika ya 19Nje! Nafasi yake ilichukuliwa na Garcia.Katika kutafuta pointi..!Kona...Martin Skrtel akitupia!!!2-0Asante!!........Skrtel akiungana na Steven Gerrard kushangilia bao hilo...Hakunaga!!! Wachezaji wa Liverpool wakipongezana..Nipishe!!!Hapa kuna penati!!wachezaji wakitofautiana punde!!David Silva aliweka 2-12-2Bora!3-2Coutinho akitupia nyaavuni bao la ushindi la tatu

No comments:

Post a Comment