Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, April 14, 2014

FULL TIME: MBEYA CITY 1 vs AZAM FC 2, AZAM MABINGWA WAPYA MSIMU HUU 2013/2014

Timu ya Azam FC imefanikiwa kutangaza Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 baada ya kuinyika Mbeya City 2-1 mjini Mbeya hii leo.

Azam FC kwa ushindi huo imefikisha pointi 59 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yeyote ile katika ligi hiyo. Azam pia mbali na kuwa bingwa pia imefikia rekodi ya Simba ya mwaka juzi ya kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Azam pia imevunja rekodi ya mwaka 2001 baada ya Ubingwa kwenda Mtibwa Suger badala ya wakongwe Simba na Yanga.

Rekodi hiyo pia inashikiliwa na timu za Coast Union ya Tanga na Tukuyu, Cosmo na Mseto Morogoro.

Yanga imeshinda mechi yake ya leo dhidi ya JKT Oljoro kwa bao 2-1 na kufikisha pointi 55, Mbeya Siti wapo nafasi ya tatu wakiwa wamebaki na pointi 46 wakifuatiwa na Simba ambayo leo nayo imepata kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Watoto wa mjini Ashanti 

United na kunusurika kushuka daraja.

MSIMAMO KWA SASA TIMU ZA JUU:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
PTS
1
Azam FC
25
17
8
0
35
50
59
2
Yanga SC
25
16
7
2
42
60
55
3
Mbeya City
25
12
10
3
12
31
46
4
Simba SC
25
9
10
6
14
40
37
MABINGWA WALIOPITA:
1965 Simba SC
1966 Simba SC
1967 Cosmopolitan
1968 Young Africans
1969 Young Africans
1970 Young Africans
1971 Young Africans
1972 Young Africans
1973 Simba SC

No comments:

Post a Comment