Timu
ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo) inatua nchini kesho mchana kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC)
dhidi ya Tanzania (Twiga Stars) itakayochezwa keshokutwa (Februari 28 mwaka
huu).
Shepolopolo
yenye msafara wa watu 29 itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka na
itafikia kwenye hoteli ya Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Waamuzi
wa mechi hiyo kutoka Burundi wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili nchini leo
asubuhi wakati Kamishna Fran Hilton-Smith kutoka Afrika Kusini atawasili kesho
(Februari 27 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South African Airways.
RAIS MALINZI
KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na
mkutano na waandishi wa habari juu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya
wakubwa (Taifa Stars).
Mkutano
huo utafanyika kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za TFF
zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.
No comments:
Post a Comment