Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 10, 2014

YAYA TOURE AWA MWANASOKA BORA AFRIKA

KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure ameshinda tunzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mara ya tatu mfululizo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, anayeng’ara katika timu ya Manchester City ya England, alipokea tuzo yake ya mafanikio ya mwaka 2013 katika usiku wa utoaji tuzo hizo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jana mjiniLagos, Nigeria.


Ameibuka kinara dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast, Didier Drogba na John Obi Mikel wa Nigeria. Toure, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2011 na 2012, alipata kura 373 dhidi ya 265 na 236 za Mikel na Drogba waliomfuatia.


Mshindi amepatikana baada ya kura zilizopigwa na makocha wakuu au Wakurugenzi wa Ufundi wa vyama na mashirikisho ya soka wanachama wa CAF.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Maofisa mbalimbali wakiwemo Rais wa CAF, Issa Hayatou, Gavana wa Lagos, Babatunde Fashola Raji Fashola, Waziri wa Vijana na Michezo Nigeria, Alhaji Bolaji Abdullah, Wajumbe wa Kamati Kuu ya CAF na wengineo.
Kwa tuzo ya mchezaji bora anayecheza Afrika, kiungo wa Misri, Mohamed Aboutrika aliwashinda wapinzani wake, Ahmed Fathy Mmisri mwenzake anayecheza naye Al Ahly na Mnigeria, Sunday Mba. 
Hiyo ilikuwa mara ya nne, Aboutrika, ambaye alitangazakustaafu Desemba mwaka jana anashinda tuzo hiyo baada ya awali kushinda mwaka 2006, 2008 na 2012.

Yaya Toure akipokea tuzo yake kutoka kwa Rais  CAF, Issa Hayatou

TUZO ZA CAF ZILIZOTOLEWA JANA:
Mchezaji Bora wa mwaka; Yaya Toure, Ivory Coast na Manchester City
Mchezaji bora wa mwaka anayecheza Afrika; Mohamed Aboutrika, Misri na Al-Ahly
Mwanasoka anayechipukia; Kelechi Iheanacho (Nigeria)
Timu bora ya mwaka; Nigeria
Timu bora ya vijana ya mwaka; Nigeria U-17 klabu bora ya mwaka; Al-Ahly (Misri)
Kocha bora wa mwaka; Stephen Keshi (Nigeria)
Refa bora wa mwaka; Haimoudi Djamel (Algeria)
Tuzo ya mchezo wa kiungwana; Mashabiki wa Nigeria
Magwiji wa CAF; Bruno Metsu, Mehdi Faria
Tuzo ya Platinum; Goodluck Jonathan (Rais wa Nigeria)
11 bora wa kuunda kombaini ya Afrika;
Kipa: Vincent Enyeama (Nigeria)
Mabeki: Ahmed Fathy (Misri), Mehdi Benatia (Morocco), Kevin Constant (Guinea)
Viungo: Jonathan Pitroipa (Burkina Faso), John Obi Mikel (Nigeria), Yaya Toure (Ivory Coast), Mohamed Aboutreika (Misri)
Washambuliaji: Emmanuel Emenike (Nigeria), Asamoah Gyan (Ghana) na Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon).

No comments:

Post a Comment