Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 31, 2013

ARSENAL WAKIFANYA MAZOEZINI KUJIWEKA SAWA MSIMU MPYA WA 2013/2014 KWENYE UWANJA WA MIZUHO PARK RUGBY


Alex Oxlade-Chamberlain kushoto akiwa na Theo Walcott
Kieran GibbsThomas Eisfeld na Ryo Miyaichi
Mikel Arteta akipeana neno na mchezaji mpya wa Gunners  aitwaye Yellowy ambaye aonekani vizuri pichaniAaron RamseyCarl JenkinsonTheo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain, Bacary Sagna na Kriss OlssonAaron Ramsey akimwaga wino kwa mashabiki.Per Mertesacker akizungukwa na mashabiki 

GARETH BALE HUENDA AKAVUNJA REKODI YENYE THAMANI ZAIDI YA CRISTIANO RONALDO NA MESSI


Touch down: Gareth Bale arrives at Heathrow Airport from Hong Kong in the early hoursTottenham Hotspur ya England imegoma kumuuza winga wake Gareth Bale kwenda Real Madrid pamoja na kupewa ya uhamisho utakaoweza kuvunja rekodi ya dunia £82million. Inasemekana Spurs kupitia mwenyekiti wake Daniel Levy wanataka walipwe kiasi hicho cha pesa pamoja na wachezaji wawili wa Real Madrid Fabio Coentrao na Angel Di Maria ambao wote kwa pamoja wana thamani ya £45m, hivyo kufanya thamani ya dili la Bale kwa jumla kuwa £126 million ambazo ni fedha nyingi sana kuliko zile alizonunuliwa Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United £80m.
Nothing to smile about: Bale, who may be subject of a world record £85m bid from Real Madrid, clearly has a lot on his mind
Bale anatarajiwa alipiwe £85m na Real Madrid kitu ambacho kitakuwa ni Historia ya Dunia kwa Kwa kuuzwa kiasi hicho kikubwa.Inasemekana pia Spurs wanataka kuongezewa wachezaji wawili tena pamoja na dau hilo nono ambalo litaweka Historia.
On his way? Gareth bale is set for talks with Spurs over a world record £85million move to Real Madrid
Gareth Bale pia anatarajiwa kuongea na Klabu yake kuhusu uhamisho huo wa £85million kwenda kwenye Klabu ya Real Madrid
Touchline: Tottenham manager Andre Villas-Boas is desperate to keep hold of his key man 

NEYMAR KUONEKANA BARCELONA MARA YA KWANZA LEO, BARCA WAKIUMANA KWENYE MECHI YA KIRAFIKI NA LECHIA GDANSK


MCHEZAJI MPYA Neymar, ataonekana kwa mara ya kwanza ndani ya Jezi ya Barcelona Uwanjani huko Poland wakati Mabingwa hao wa Spain watakapocheza Mechi ya Kirafiki na Lechia Gdansk Siku ya Jumatano.
Mechi hii ilikuwa ichezwe mapema Mwezi huu lakini ilifutwa mara baada ya kutangazwa kuondoka kwa Meneja wa Barcelona, Tito Vilanova, kwa matatizo ya maradhi ya Kansa.
Kikosi ambacho kitacheza huko Poland kina Vijana wengi lakini pia wapo Lionel Messi, Cristian Tello na Alex Song na kitaongozwa na Kocha Msaidizi, Jordi Roura, huku Kocha mpya Tata Gerardo Martino akibaki Barcelona na Wachezaji wengi wa Timu ya Kwanza waliochelewa kurudi Mazoezini baada ya kuongezewa Likizo kwa vile walicheza Kombe la Mabara huko Brazil Mwezi uliopita.
Neymar wakati anatambulishwa Barca siku za nyuma kidogo 

RATIBA SERIE A MSIMU WA 2013/14 HA!! MABINGWA JUVE KUANZA UGENINI NA SAMPDORIA!!



Juventus wakishangilia RATIBA ya Msimu mpya wa Ligi ya Italy, Serie A, imetoka na Mechi za ufunguzi ni Wikiendi ya Agosti 24 na 25 na Mabingwa Watetezi Juventus wataanza ugenini na Sampdoria, Timu pekee ambayo iliwafunga nje ndani Msimu uliopita.Ligi hiyo itamalizika hapo Mei 18 Mwaka 2014.
Ratiba hiyo, iliyoandaliwa na Kompyuta, ilitolewa leo huko Mjini Milan katika sherehe maalum.
Katika Msimu huu mpya zipo Dabi 5 za Miji ya Milan, Rome, Turin, Genoa na Verona lakini Ratiba zake zimehakikisha Mechi zake hazipangwi katikati ya Wiki kwa sababu za Kiusalama.
Pia, Klabu ambazo zimo Mashindano ya UEFA, CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI, zimetenganishwa zisikutane zile Wiki kabla ya Mechi zao za UEFA. 

MAJIMAJI KUWA KAMPUNI KUANZIA MSIMU HUU

TAFADHALI POKEA TAARIFA KUHUSU MAJIMAJI REVIVAL CONFERENCE  
INAYOFANYIKA TAREHE 10.08.2013 YENYE LENGO LA KUIFANYA MAJIMAJI FC  
KUWA KAMPUNI NA KUWEZESHA KUIRUDISHA LIGI KUU TANZANIA BARA!

MKUTANO UTAKUWA CHINI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA HUKU WATOA MADA WAKIWA  
NI WAKALA WA KIMATAIFA WA FIFA DKT DAMAS NDUMBARO NA BWANA SILAS  
MWAKIBINGA.

KAMA KUNA TAARIFA YA ZIADA AMBAYO ITAHITAJIKA TAFADHALI WASILIANENI NA  
MSEMAJI TULIYEMTEUA BWANA NASIBU MAHINYA 0655 468800.

NI MAPINDUZI MAPYA KATIKA SOKA NA KUIFANYA MAJIMAJI FC KUWA MFANO WA  
KUIGWA KWENYE UENDESHAJI NA UZALISHAJI WA VIPAJI TANZANIA KWAAJILI YA  
KUUZWA NJE YA NCHI.

KAZI NJEMA

Teonas Aswile
Managing Director,
Tanzania Mwandi Co Ltd.
Phone: +25522 2120677 or +255756 829071
Fax: +255 22 2122976
Email: ceo@tanzaniamwandi.co.tz,
info@tanzaniamwandi.co.tz
Website: www.tanzaniamwandi.co.tz/events.html

RATIBA LIGI DARAJA LA KWANZA AGOSTI 14


Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2013/2014 inayoshirikisha timu 24 zilizo katika makundi matatu zikicheza kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) inatarajiwa kutolewa Agosti 14 mwaka huu.

Kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).

African Lyon (Dar es Salaam), Friends Rangers (Dar es Salaam), Green Warriors (Dar es Salaam), Ndanda (Mtwara), Polisi (Dar es Salaam), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam) zinaunda kundi B.

Timu za kundi C ni JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).

Tunapenda kukumbusha kuwa dirisha la usajili kwa madaraja yote ni moja ambapo usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati hatua ya pili ni Agosti 14 hadi 29 mwaka huu. Dirisha dogo litafunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.

WAAMUZI VPL KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI

Waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) utakaofanyika katika vituo viwili.

Mtihani huo utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es Salaam na Morogoro. Kituo cha Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.

Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki katika mtihani huo.

MTIHANI WA UWAKALA WA WACHEZAJI, MECHI SEPT 26


Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

Mtihani huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

MASHINDANO YA MOSCOW KUWA MWISHO WA UFALME WA USAIN BOLT?

NDIYE mwanariadha mwenye kasi kuliko mwanariadha yeyote tangu kuanzishwa kwa mashindano ya riadha mwaka 1977. Sekunde 9.58, alizotumia katika mbio za mita 100, mwaka 2009 huko Berlin, unabaki kuwa muda mfupi katika vitabu vya Shirikisho la Riadha, IAAF.
Licha ya kushiriki mashindano mbalimbali, lakini rekodi hii inabaki kuwa ya kipekee. Katika mashindano ya Olimpiki ya 2012, Bolt aliahidi angeifikia kama si kuvunja kabisa rekodi hiyo, lakini hakufanikisha hilo, zaidi aliandikisha rekodi ya Olimpiki, kwa kutumia sekunde 9.63 katika mita 100.
Umaarufu wake umepambanua mpaka kwenye mbio fupi za mita 200 na zile za kukabidhiana vijiti 4×100m.
Kwa kifupi, tangu 2008, katika mashindano ambayo Bolt ameshiriki, medali za dhahabu zimepelekwa Jamaica. Na katika mashindano ya mwaka huu, gwiji huyo hakufanya makosa, alihakikisha medali za dhahabu zinapelekwa Jamaica, ikiwemo ya mbio za kukabidhiana kijiti.
Naam, huyo ndiye Usain St. Leo Bolt, miaka 26, mzaliwa wa Trelaway, Jamaica, ingawa baadae, aliamua kukimbia kijiji na kuhamia jijini Kingston.
Bolt, tayari amemaliza kazi aliyotumwa na taifa lake huko Uingereza-kurejesha heshima ya medali za dhahabu.
Kizingiti kimebaki kimoja tu, kuhakikisha anatetea heshima yake kwenye mashindano ya dunia yatakayoanza kutimua vumbi -Moscow Urusi Agosti 10-18. Mashindano ambayo yatawakosa wapinzani wakuu wa Bolt, Asafa Powell, Mjamaica mwenzake na Mmarekani Tyson Gay, waliofungiwa kwa tuhuma za kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Gay, anashikilia nafasi ya tatu, nyuma ya Yohan Blake, kwa kuwa na rekodi ya kukimbia sekunde 9.71 huko Berlin Ujerumani, 2008 katika mashindano ya dunia mita 100. Huku Powell yeye anashika nafasi ya nne kwenye orodha hiyo ya ‘wakimbiza upepo’ maarufu duniani kwa rekodi ya kutumia  sekunde 9.72 Uswisi mwaka 2008.
Lakini licha ya kukosekana wakongwe hao (wote miaka 30), sio kigezo cha Bolt kutohofia upinzani, kwani kizazi kipya cha kina Yohan Blake kimekuja juu na lolote linaweza kutokea.
Hofu ya mashindano ya Moscow
Mashindano ya dunia yanatarajia kuanza kutimua vumbi mwezi ujao huko Moscow Urusi, ambapo tayari Bolt amethibitisha kuiwakilisha Jamaica kama si kutetea heshima yake. Lakini kigezo cha umri ambao kwa namna moja ama nyingine umeanza kumtupa mkono-miaka 26, kinaweza kuchukuliwa kama kigezo kikubwa cha gwiji huyo kushindwa kufurukuta mbele ya Yosso kina Blake (miaka 23) na Delano Williams (19).
Blake, kitendo cha kuvunja rekodi ya Gay, kinaashiria ni wakati wa damu changa na kusahau kile cha Tyson Gay, Asafa Powell, Olusoji Fasuba, na sasa Bolt taa zimeanza kuwaka kuashiria kufikia mwisho wa utawala.
Hivi karibuni Bolt alikiri kuwepo na upinzani mkubwa katika kizazi kipya, baada ya kushuhudia ‘dogo’ Delano Williams akifanya maajabu kwenye mashindano ya mita 200, huko Uingereza, pamoja na kutwaa medali ya dhahabu kwa vijana mwaka jana.
“Siachi kusema Williams atakuwa tishio duniani, maana ni mdogo na ni mpiganaji,” alisema Bolt.
Nguvu ya madawa
Imegundulika kuwa Bolt anatumia nguvu yake asilia, hivyo rekodi alizoandikisha katika tasnia hii, ni nguvu yake, tofauti na Gay na Powell ambao walidiriki kutumia njia za mkato kutafuta umaarufu.
Vipimo vilivyofanywa na Shirika la kupambana na utumizi wa madawa, USADA Mei mwaka huu, vilidhihirisha kuwepo kwa idadi kubwa ya wanariadha wanaotumia nguvu ya ziada huku idadi kubwa ikiwa ni Wajamaica.
Kuna kipindi alizushiwa kutumia madawa, lakini majibu ya vipimo vilivyochukuliwa wiki za hivi karibuni, vilibainika Bolt hatumii ‘nguvu ya ziada’.
Bolt na ufalme ya riadha
Pamoja na Gay na nduguze kutumia madawa ya nguvu za ziada, lakini hakuna aliyefanikisha kufikia rekodi ya gwiji huyu, labda Gay kidogo alijaribu kwa kutumia sekunde 9.75 mwaka huu huko Des Moines, Marekani.
Bolt, maarufu kama ‘Lighting Bolt’ mbali na rekodi hiyo ya mita 100, anashikilia rekodi ya kutwaa medali nyingi za dhahabu, ambapo ametwaa jumla ya medali 30, zikiwemo sita za mashindano ya dunia, tangu 2001 alipojiunga rasmi na mchezo huu.
Mwaka 2009, ulikuwa wa neema kwa Bolt pia, aliandikisha rekodi kwenye mbio za mita 200 kwa kutumia sekunde 19.19 Berlin Ujerumani, kabla ya 2012 kuwaongoza Yohan Blake, Michael Frater na Nesta Carter kuweka rekodi mpya kwenye mbio za kukabidhiana akijiti katika mashindano ya Olimpiki London-Uingereza 36.84.
Ni kwenye Olimpiki hizo, sekunde 9.63, zilimfanya Bolt kuandikisha rekodi mpya ya Olimpiki. Hiyo ilimfanya kushikilia rekodi zote za mchezo wa riadha kwa mbio fupi-Mashindano ya dunia na yale ya Olimpiki.
Swali linabaki je, Bolt ataweza kutetea medali zake huko Moscow? au ndio tuseme ni muda sasa wa damu changa ya kina Blake kumuondoa ‘mkoloni wa raidha’ ambaye amejitangaza kuwa mwasisi wa riadha muda wote.
Kifuta jasho: Powell alikuwa tishio kwa kutwaa medali za dhahabu wakati wa ujana wake kati ya miaka 21-25, vivyo hivyo kwa Gay, mpaka wanafungiwa wakiwa na miaka 30, hawakuwa na jipya, licha ya kusaidiwa na madawa kama inavyodaiwa. Picha inayojengeka kwa Bolt huenda asifurukute kwa Blake katika mashindano ya Moscow kutokana na umri.
Yetu macho, kwa hisani ya Supersport, tunangojea kwa hamu kumuona Bolt mbele ya Blake.
KUMBUKUMBU YA UWANJA
Mashindano ya mwaka huu yatafanyika kwenye dimba la Luzhniki Moscow, lenye  rekodi nzuri kwa mashabiki wa Man United, kwa kumbukumbu ya kutwaa kombe la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) dhidi ya Chelsea, kwa njia ya penalti. Juni 25, 2008 ni tarehe ambayo kamwe United hawawezi kuisahau, si kwa timu wala mashabiki tu, bali hata Kibabu Alex Ferguson (aliyekuwa kocha wake), kwani Luzhniki ndilo dimba la mwisho katika maisha yake ya soka, lililompatia ubingwa wa mwisho wa michuano hii, ikiwa ni mara ya tatu, akiwa kama kocha wa United ndani ya miaka 26 kabla ya kustaafu msimu uliopita.
Kwa upande mwingine, ni uwanja wenye chuki na watu Chelsea, hususan nahodha John Terry na aliyekuwa mshambuliaji wao, Nicolaus Anelka, walioshindwa kukwamisha nyavu zao na kuwapa ubingwa mahasimu zao. Dili la United kidogo ‘libumishwe’ na nyota wake, Cristiano Ronaldo, aliyekosa penalti ya tatu, lakini kushindwa kwa Terry kukwamisha mkwaju wa tano kwa Chelsea, ndio ulikuwa ukombozi wa Ferguson.

Wawakilishi wetu
Hakuna sura ngeni kwa upande wa  wawakilishi wa Tanzania, ni zile zile zilizoshiriki mashindano ya Olimpiki mwaka jana huko London, England. Faustine Mussa, Samson Ramadhani na Daudi Msenduki na msichana Zakia Mrisho, ndizo sura nne zinazotajwa kuliwakilisha taifa lenye idadi ya watu wapatao milioni 45, lakini pia huenda ikapungua kwa mujibu wa ripoti zilizopo. Ni idadi inayoshtua kidogo, ikilinganishwa na idadi ya taifa zima, ama kulinganisha na mataifa mengine yenye wawakilishi wengi.
Lakini cha kushangaza, pamoja na uchache huo, si wawakilishi labda pengine wanaweza kuwapa matumaini taifa kurejea na medali, kutokana na rekodi zao kwenye mashindano ya London. Tanzania iliishia kuwa kwenye vitabu vya ushiriki wa Olimpiki, kutokana na kwamba Mussa na Ramadhani walimaliza katika nafasi za mbali za 33 na 66, ambazo hii leo Mtanzania hawezi kujipa matumaini ya kurejea na medali. Vivyo hivyo kwa Mrisho, hali ilikuwa tete London pamoja na wawakilishi wa mchezo wa kuogelea na Seleman Kidunda kwa upande wa ngumi.
Ripoti zilizopo ni kwamba huenda Ramadhan asishiriki kutokana na kigezo cha umri kumtupa mkono, wakati Zakia, ambaye walau mashindano ya 2011 huko Daegu Korea Kusini alimaliza katika nafasi ya 11 kwenye mbio za mita 5,000, naye anaweza asiende ‘kwa kina Arshavin’ kupeperusha bendera. Dukuduku linabaki je, Tanzania haina vipaji vingine mpaka kuwakilishwa na watu wanne kati ya milioni 45?

NYOTA WATANO WALIOTABIRIWA MAKUBWA ITALIA LAKINI WAKASHINDWA

MILAN, Italia
KATIKA vitabu vya timu ya taifa ya Italia ya wanaume, kuna majina ya wanasoka nguli waliopata kung’ara na kikosi hicho, aidha kwenye michuano ya Ulaya ama fainali za dunia. Nyota kama Paolo Maldini, Franco Baresi, Alessandro Del Piero na Francesco Totti, ni baadhi ya waasisi wa soka kwa taifa la Italia na ulimwengu kwa ujumla.
Baada ya kizazi cha kina Baresi, Maldini na Totti na kina Del Piero, ni muda wa kina Andre Piero na kipa Gianiluig Gig Buffon ambao wako ukingoni mwa soka, kupigana kufa kupona kuhakikisha wanafikia ‘level’ za magwiji waliopita.
Wakati kina Maldin na nduguze wakiandikisha wasifu heshima, kwa upande mwingine kuna nyota walioonekana kurithi fimbo zao, lakini ghafla hawakufikia malengo yao, kwa sababu za hapa na pale.  
Kwa msaada wa mitandao ya kimataifa, Dimba, ilichambua nyota wa Kiitaliano ambao walipigiwa upatu na wadau, wachambuzi wa masula ya soka, ambao pengine wangekuwa waasisi wa taifa la kesho, ingawa ndoto zao zilipotelea kusikojulikana. Hii ni orodha ya wanandinga hao.
Alberto Aquilani
AS Roma, inaaminika kwa kusaka, kukuza na kutunza vipaji vya wachezaji wazawa. Nyota kama Francesco Totti na Daniele De Rossi, walikulia na kupatia umaarufu mkubwa wakiwa Roma. Alessandro Florenzi katika kizazi kipya ndiye anatabiriwa kuwa lulu ya taifa kutoka klabu ya Roma.
Ndivyo ilivyokuwa msimu wa 2000 kwa Alberto Aquilani, alivyochipukia katika klabu ya Roma. Kiwango chake kilizitoa udenda timu kubwa, zikiwemo Chelsea na Arsenal zilizomtangazia ofa nzuri, lakini aliikacha ofa hiyo na kubaki Roma.
Aliiwezesha Roma kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa wa Serie A, mara mbili 2005 na 2006, rekodi iliyopitwa na Inter Milan baadaye-waliochukua mara tatu.  Pole pole Aquilani alianza kupotea katika ramani ya soka kutokana na majeraha ya muda mrefu katika msimu wa 2006-07, lakini jeraha alilopata msimu wa 2008-09, ndilo lilizima ndoto ya kufikia mafanikio ya kina Totti na Del Piero.
Majeruhi aliyopata katika mechi ya Klabu bingwa Ulaya dhidi ya Chelsea 2008, yalimuweka nje takribani msimu mzima, lakini alirejea uwanjani baadaye, kabla ya Februari kupata jeraha jingine kubwa zaidi lililomuweka nje msimu mzima.
Msimu 2009, Roma iliamua kumpiga bei kwa majogoo wa Anfield, Liverpool, kwa uero mil. 20, kwa matarajio kuwa angekuwa mbadala wa Xabi Alonso aliyetimkia Real Madrid, lakini hakuonekana uwanjani mpaka Novemba.
Visa na mikasa ilianzia hapo na hakuwa tena na uwezo wa kucheza dakika 90 kama enzi zake pale Roma. Kuondoka kwa kocha Benitez, ndoto ya Aquilani kupata namba kwenye kikosi cha kocha mpya, Roy Hodgson, zilikuwa finyu na kuamua kumtoa kwa mkopo Juve.
Kidogo alipata nafuu pale Juventus, ingawa hawakuwa tayari kumnunua.  Kumalizika kwa mkopo huo, Liver ilimpeleka AC Milan kwa mkopo tena, lakini janga la majeruhi liliendelea kumuandama tena.
Msimu uliopita, alijunga na Fiorentina ambapo kiwango chake kidogo kirejee, lakini licha ya kuitwa kwenye timu ya taifa kwenye michuano ya mabara mwaka huu, kiwango chake si kile jamii ya mpira ilitarajia enzi za ujana wake na kamwe hawezi kufikia mafanikio ya kina Baresi.
Amauri
Mshambuliaji mwenye asili ya Brazil, msimu wa 2007/8 alikuwa na nyota nzuri, baada ya kuifungia Palermo mabao 15 kwenye Ligi kuu Serie A, kiwango kilichoanza kuzitoa mate  vigogo. Ilikuwa ni Juventus, iliyomnasa kwa kumfanya ‘swap’, dili-mbadilishano, kwa kuwapa Antonio Nocerino na kiasi cha euro milioni 22.8.
Lakini pamoja na upinzani wa namba Turin mbele ya wakali Alessandro Del Piero, David Trezeguet na Vincenzo Iaquinta, bado Amauri alifunga jumla ya mabao 14, huku mabao mawili akiyafunga kwenye mechi 10!
Pole pole, alianza kupotea msimu hadi msimu.  Katika msimu wa 2009/10, aliishia kuzifunga timu tano tu kati ya timu 30 alizokutana nazo, huku msimu uliofuata akicheza mechi tisa na kushindwa kufunga bao hata moja.
Ujio wa Antonio Conte kama kocha wa Juve, ndio kabisa Amauri alikufa jumla.  Alilazimika kupigwa bei kwa Fiorentina msimu wa 2011 kwa bei ‘ya nyanya’, euro 500,000, ikiwa na hasara ya uero mil. 22.3.
Amauri alitoa mchango mkubwa kwa Fiorentina, bao la ushindi kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AC Milan, lilitoa mwanya kwa Juve kutwaa ubingwa wa Serie A kwa kuwaacha wapinzani, Milan pointi nyingi.
Imebaki kuwa historia kwa Amauri, kuwa aliwahi kuwa kwenye kiwango kizuri, lakini kujiunga na Juve, ulikuwa mwanzo wa majanga, na hana namba kwenye timu ya taifa tena. Msimu uliopita alifunga mabao 10 kwenye mechi 33 alizoichezea Parma alipo kwa sasa.
Alberto Gilardino
Akiwa na miaka 23, Alberto Gilardino alikuwa mmoja wa nyota waliotikisa dunia, ikiwemo kuiwezesha Italia  kutwaa ubingwa wa Dunia 2006.  Hii leo ana miaka 31, ameacha mshangao mkubwa kwa wadau wa soka.
Gilardino, alitikisa soka la Kiitalia, mabao yake 50 katika mechi 96 alizoichezea Parma tangu 2002/05, yaliwaumiza vichwa vigogo nchini humo, na Rais wa AC Milan, Silvio Berlusconi, hakuwa na kigugumizi cha kutoa euro mil. 25 kuhakikisha anachezea Milan.
Katika misimu yake mitatu pale Milan, Gilardino alijijengea heshima kubwa kwa ufumaniaji wa nyavu, hasa katika michuano ya Klabu bingwa Ulaya, ukiwemo msimu wa 2006-07, alipokuwa lulu ya ubingwa wa UEFA. Ndiye aliizamisha Manchester United nusu fainali, kabla ya kuwapa ubingwa Milan akitokea benchi na kufunga bao la  ushindi wa 2-1 dhidi ya Liverpool kwenye mechi ya fainali.
Pamoja na hayo, bado hakuwa Gilardino yule wa Parma, msimu uliofuata 2008, alijiunga na Fiorentina kwa hasara ya euro mil.10. Ulikuwa uhamisho wa maana kwake, alikutana na kocha wake wa zamani, Cesare Prandelli, aliyekuwa kocha wa Parma, na msimu wake wa kwanza alifunga mabo 25 katika michuano yote.
Nyota ya mikosi ilianza kumuandama polepole, kuondoka kwa Prendeli aliyejiunga na timu ya taifa, alipigwa bei kwa Genoa iliyokuwa daraja la pili, kabla ya kuhamia Bologna msimu 2012 ambapo alifunga mabao 13 katika mechi 36.
Lakini pamoja na kushuka kiwango, ana kila sababu ya kumshukuru Prandelli, aliyempendelea kwenye timu ya taifa. Bado anamthamini na alijumuisha kwenye kikosi kilichoshiriki kombe la mabara na kumpa nafasi ya kuziba pengo la Mario Balotelli baada ya kuumia.
Tangu awe na msimu mzuri na Parma wakati akiwa yosso, Gilardino alitarajiwa kuwa tishio hata zaidi ya kina Baresi na Roberto, lakini njia aliyopitia haikuwa ya mafanikio, na sasa ni babu asiyeweza kufanya cha ajabu.
Antonio Cassano

Utukutu wa Antonio Cassano, si kigezo cha kuzima kipaji chake. Cassano hana rekodi nzuri kwa klabu alizochezea, kutokana na adhabu alizokumbana nazo.
Kizingiti cha kwanza ni alipokuwa na Roma, baada ya kumbeza mwamuzi Roberto Rosetti wakati alipotolewa nje. Kitendo hicho kiliwaudhi viongozi wa Roma na mwishowe kuuzwa Real Madrid msimu wa 2006 kwa ada ya euro mil. 5, ikiwa ni hasara ya euro mil. 25, walizomnunua kutoka Bari.
Alipotua Real, alikumbana tena kocha Fabio Capello, aliyetokea Roma na ‘kumpiga pini’ na baadaye kuamua kurejea Ligi ya Italia kujiunga na Sampdoria kwa mkopo.
Ushirikiano wake na Giampaolo Pazzini waliiwezesha Sampdoria kucheza Klabu bingwa Ulaya - moja ya mafanikio makubwa kwa timu hiyo.
Msimu wa 2010, alikumbana na kisanga kingine, baada ya kuadhibiwa na Mwenyekiti wa Sampdoria, Riccardo Garrone, baada ya kukataa kuhudhuria sherehe za tuzo. Cassano alifungiwa kucheza kikosi cha kwanza, hivyo kuuzwa AC Milan msimu wa 2011.
Cassano, licha ya kuwa na kiwango kizuri msimu wa 2011/12, alikumbana na matatizo ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva, naye alivuka mitaa miwili, mitatu na kujiunga na Inter Milan kwa kubadilishana na Giapolo Pazzini.  
Utukutu wake umemfanya awe mtu wa kuhamahama, tayari msimu huu amepelekwa Parma, haijawekwa wazi kama ‘alizikunja’ na Kocha wa Inter, Andrea Stramaccioni, hadi kumuuza, lakini inahisiwa huenda kuna janga alitenda. Hahami hivi hivi.
Ni matendo hayo, yamemfanya kushindwa kufikia mafanikio ya kina Maldini, aidha kwenye klabu ama timu ya taifa, licha ya kuwa na kiwango kizuri.

Fabio Quagliarella

Baada ya kuapa kujituma mpaka apate namba kwenye kikosi cha taifa, Fabio Quagliarella hatimaye ndoto yake ilitimia msimu wa 2006/7, kufuatia mabao 13 aliyofunga akiwa na klabu ya Sampdoria msimu wa 2006-07.  
Lakini uhamisho wake kwenda Udinese, uligubikwa na utata mkubwa baina ya timu hizo, hata hivyo ni Udinese ilishinda kesi hiyo. Katika misimu miwili, alifunga mabao 25 katika michezo 73 na kuisaidia Udinese kufuzu kucheza Ligi ya Ulaya msimu wa '08-09.
Baadaye alihamia klabu ya nyumbani ya Napoli, lakini ujio wa nyota wa Uruguay, Edinson Cavani kutoka San Paolo, alizima nyota ya Quagliarella.
Ujio wa Cavani, ulikuwa ni mwanzo wa kupotea kwa nyota huyo, kwani licha ya kuitwa kwenye michuano ya dunia 2010 huko Afrika Kusini, hakupata nafasi, zaidi aliishia kucheza dakika 45 tu kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Slovakia.

Licha ya Italia kushindwa kufuzu, lakini bao lake katika mchezo na Slovakia, lilikuwa moja ya mabao matano ya michuano hiyo.
Kiwango ndani ya dakika 45 hizo, ziliwashawishi Juventus kumchukua kwa mkopo. Aliifungia Juve mabao tisa ndani ya nusu msimu, lakini maisha yalianza kuwa magumu baada ya kupatwa na jeraha la goti.
Kabla ya kupatwa na jeraha hilo, alitabiriwa kuwa nyota mpya ya Italia ambaye angeweka rekodi kama wasisi waliopita, lakini majeraha ya hapa na pale yamepelekea kutokuwa na namba kwenye kikosi cha taifa.


Monday, July 29, 2013

YANGA YAKATAA MECHI ZAKE ZISIONYESHWE NA AZAM TV

YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
1.      bodi ya TPL
1.1  Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2  Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3  Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2.      utaratibu wa dunia nzima
2.1  Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.
2.2  Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie  urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.
2.3  Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania  watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4  Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1        Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2        Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3        Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3.      MIGOGORO YA MASLAHI

3.1   Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na  kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2  Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira  wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3   Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4.      KUTOKUWA NA UWAZI
4.1   Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari,  na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2   Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.

5.      Mazingatio ya kibiashara
5.1  Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia  kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2  TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji  wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.

Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA  Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji)  walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
 
………………………………………..
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
Young Africans Sports Club
29 JULAI, 2013

RHINO RANGERS YAMTEUA SEBASTIAN NKOMA KUWA KOCHA MKUU


UONGOZI wa timu ya soka ya Rhino Rangers ya Tabora umemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Renatus Shija aliyetimuliwa wiki iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu leo, Katibu wa Rhino Rangers, Clarence Kambona alisema kuwa wamemchukua Sebastian kwa kuwa ni kocha makini na mwenye mafanikio kwenye ufundishaji wa soka.

“Kutokana na maazimio ya kikao kilichokaa baada ya kuondolewa madarakani makocha wetu, uongozi ulimteua Sebastian kuifundisha timu yetu ambayo kwa sasa iko katika maandalizi ya msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu, na msaidizi wake atakuwa Emanuel Gift,” alisema Kambona.

Rhino iliwatupia virago makocha wake Renatus Shija na Hamadi Mgongo waliopandisha daraja timu hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na viwango vya kufundishsa timu za Ligi Kuu.

Kocha mpya wa Rhino kwa mara ya mwisho alikuwa anafundisha timu ya Jamhuri ya Pemba ambayo ili iliwakilisha nchi kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika.

MAN UNITED YATOA KIPIGO LEO HONG KONG



Hong Kong, China
MABINGWA wa Ligi Kuu England, Manchester United leo walifuta mzimu wa kufanya vibaya ziara yao ya Mashariki ya Mbali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya klabu ya Kitchee ya Hong Kong.

Mabao ya vijana wa David Moyes kwenye pambano hilo yaliwekwa kimiani na straika wake Danny Wellbeck katika dakika 16 ya mchezo baada ya kazi nzuri iliyofanywa na winga wa timu hiyo, Ashley Young. 

Ikishambulia kwa kasi, Man United ilipata bao la pili kupitia kwa beki wake Chris Smalling katika dakika 22 baada ya kuunganisha wavuni krosi iliyopigwa na Tom Cleverley, kabla ya Fabio da Silva kupachika bao la tatu hivyo kumaliza kipindi cha kwanza ikiongoza kwa mabao 3-0.

Man United ilikianza kipindi cha pili kwa kasi, ambapo shambulizi lake la kwanza lilizua bao katika dakika ya 47 mfungaji akiwa  kiungo chipukizi Adnan Januzaj, kabla ya Lingard kupachika bao la tano.

Wenyeji walipata mabao yao kupitia kwa Lam Kai Wai katika dakika ya 53 na Alex Alkande katika dakika ya 69, katika mchezo huo ambao awali Man United walitaka kugoma kucheza kutokana na ubovu wa sehemu ya kuchezea ya uwanja uliotumika.

Matokeo ya Man United kabla ya mechi ya Jana, walipigwa 1-0 na Singha All Stars, wakashinda 5-1 dhidi ya A-League All Stars, wakapigwa 3-2 na Yokohama F-Marinos, kabla ya kutoa sare ya 22 na Cerezo Osaka katika mechi yake ya mwisho.