Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, July 29, 2013

MAN UNITED YATOA KIPIGO LEO HONG KONG



Hong Kong, China
MABINGWA wa Ligi Kuu England, Manchester United leo walifuta mzimu wa kufanya vibaya ziara yao ya Mashariki ya Mbali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya klabu ya Kitchee ya Hong Kong.

Mabao ya vijana wa David Moyes kwenye pambano hilo yaliwekwa kimiani na straika wake Danny Wellbeck katika dakika 16 ya mchezo baada ya kazi nzuri iliyofanywa na winga wa timu hiyo, Ashley Young. 

Ikishambulia kwa kasi, Man United ilipata bao la pili kupitia kwa beki wake Chris Smalling katika dakika 22 baada ya kuunganisha wavuni krosi iliyopigwa na Tom Cleverley, kabla ya Fabio da Silva kupachika bao la tatu hivyo kumaliza kipindi cha kwanza ikiongoza kwa mabao 3-0.

Man United ilikianza kipindi cha pili kwa kasi, ambapo shambulizi lake la kwanza lilizua bao katika dakika ya 47 mfungaji akiwa  kiungo chipukizi Adnan Januzaj, kabla ya Lingard kupachika bao la tano.

Wenyeji walipata mabao yao kupitia kwa Lam Kai Wai katika dakika ya 53 na Alex Alkande katika dakika ya 69, katika mchezo huo ambao awali Man United walitaka kugoma kucheza kutokana na ubovu wa sehemu ya kuchezea ya uwanja uliotumika.

Matokeo ya Man United kabla ya mechi ya Jana, walipigwa 1-0 na Singha All Stars, wakashinda 5-1 dhidi ya A-League All Stars, wakapigwa 3-2 na Yokohama F-Marinos, kabla ya kutoa sare ya 22 na Cerezo Osaka katika mechi yake ya mwisho.

No comments:

Post a Comment