Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 20, 2013

WACHEZAJI 10 ULAYA AMBAO WAREMBO WANAWAZIMIKIASOKA ndiyo mchezo unaopendwa zaidi duniani, kutokana na umaarufu wa mchezo huo kuwafanya wachezaji wake kuwa kivutio kila kona duniani.

Sifa moja ya wachezaji wa soka ni ukakamavu wa kimichezo walionao, kitendo cha miili yao kujengeka kimichezo kimewafanya wawe kivutio kikubwa cha warembo duniani kote.

Mademu wakali wamekuwa wakihaha kusaka nafasi ya kuonja penzi la nyota hao kutokana na mvuto walionao.Kwa hapa Bongo, msanii wa Bongo Fleva, Diamond, ndiye anajulikana kama asali ya warembo, kutokana na wasichana wengi kumpapatikia.Lakini kwa upande wa ng’ambo, wanasoka wamekuwa wakiongoza kuwanasa warembo na wafuatao ni nyota 10 wenye mvuto zaidi.

 

10. Wesley Sneijder

Wesley Sneijder ni nyota wa Uholanzi, anayekipiga Galatasaray. Kiukweli ni mchezaji mwenye kipaji na zaidi kutokana na uwezo wake wa kutumia miguu yake yote miwili.

Nyota huyo naye yumo katika orodha ya wachezaji wenye mvuto kwa warembo.

 

9. Lionel Messi 

Nyota huyo ambaye amenyakua tuzo ya uchezaji bora mara nne, kutokana na kipaji chake cha hali ya juu na yeye yumo katika orodha ya wachezaji wenye mvuto.

Ingawa hana tabia ya kuranda na warembo na haonekani kuwa na muonekano mzuri, lakini kiwango chake kimekuwa kikiwashawishi warembo watake kumnasa.

 

8. Xabi Alonso

Akiwa na urefu wa miguu sita, na yeye ni kati ya wanasoka 10 ambao ni asali ya warembo.

Alonso, aliyetokea eneo la Basque nchini Hispania, anajulikana kwa uwezo wake wa kupiga pasi za ufundi na pia amekuwa akitunza muonekano wake na kuwateka warembo kibao.

 

7. Mario Gomez

Nyota wa Ujerumani, Mario Gomez, anayekipiga Fiorentina, pamoja na uwezo wake wa kupasia nyavu, pia ni asali ya warembo.

Gomez siyo tu ana sifa ya kupachika mabao na kuwa kivutio cha mademu, bali pia amekuwa akijishughulisha na masuala ya kijamii.

Amewahi kuzungumzia mapenzi ya jinsia moja na kuwahamasisha wachezaji mashoga kujieleza ili wajisike huru kutandaza soka.

6. Theo Walcott

Mara nyingi amekuwa hahesabiwi sana katika wanasoka wenye mvuto kwa wasichana, lakini ukiangalia sura yake utagundua kuwa anastahili kuwemo kwenye orodha hii.

Walcott ni mvulana mtulivu anayejiheshimu, labda ndiyo maana amekuwa hahusishwi katika orodha ya wanasoka wenye mvuto.

Winga huyo wa Arsenal, ambaye juzi aliifungia timu hiyo bao la kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Marseille wakati wa Ligi ya Mabingwa, Juni mwaka huu alimuona rafiki wake wa siku nyingi, Melanie Slade.

 

5. David Beckham

Pamoja na kustaafu soka, lakini David Beckham atabakia kuwa kivutio cha warembo miaka yote kwenye mchezo huo.

Huenda kama si ulinzi mkali kutoka kwa mke wake, Victoria, angeendelea kuwa kicheche, kutokana na warembo wengi wamekuwa wakisaka penzi la nyota huyo wa England.

 

4. Iker Casillas

Iker Casillas ni mmoja wa walinda milango walioanza kukaa langoni wakiwa wadogo na kufanya vizuri kazi yake.

Muonekano wake na kile anachofanya akiwa langoni, kimekuwa kishawishi kikubwa kwa warembo.

 

3. Mesut Ozil

Macho yake ni mvuto tosha kwa warembo, huhitaji kuangalia muonekano wake na mwendo wake.

Ozil, ambaye amesajiliwa na Arsenal msimu huu na kuvunja rekodi ya kununuliwa kwa pauni milioni 42.5.

Nyota huyo wa Ujerumani, amefanikiwa kuwateka warembo kama Anna-Maria Lagerblom na mpenzi wake wa sasa, Mandy Capristo, ambaye ni mwanamitindo na mwimbaji wa Ujerumani.

 ricardo kaka photo: Ricardo Kaka 76dd59d6.jpg

2. Ricardo Kaka

Nyota aliyerejea kwenye klabu yake ya AC Milan, Ricardo Kaka, ana muonekano wa ‘kimodo’ na sura ya kitoto inayowateka warembo wengi.

Kama si tabia yake ya kupenda dini, basi angekuwa ana lori lililojaa warembo kutokana na muonekano wake na mwili wake ulivyo.

 

1. Cristiano Ronaldo

Huyu ndiye funga kazi. Ana muonekano mzuri na mwili wenye misuli iliyojazia na kuwavutia warembo wengi.

Tabia yake ya ukicheche, imewafanya wasichana wanase penzi lake kwa urahisi, ingawa amekuwa akichagua wasichana wenye viwango na maarufu kama akina Kim Kardashian, Paris Hilton, Maria Sharapova na Raffaella Fico, ambaye alikuwa ‘demu’ wa Mario Balotelli.

Wengine aliotembea nao ni akina Jordana Jardel, Karina Ferro, Daniele Aguiar, Isabel Figueir, Diana Chaves, Nuria Bermudez,

Soraia Chaves, Merche Romero, Luciana Abreu, Gemma Atkinson, Bipasha Basu, Karina Bacchi, Carolina Patrocinio, Lucia Garcia, Niki Ghazian , Tyese Cunningham, Nereida Gallardo, Mia Judaken, Imogen Thomas, Letizia Filippi, Alyona Haynes, Olivia Saunders, Gabriela Endringer na Luana Belletti.

No comments:

Post a Comment