YANGA
inatarajia kuondoka kesho alfajiri kwenda Mbeya kuweka kambi ya kujiandaa na
mchezo wa ngao ya jamii, huku wapinzani wao, Azam FC nao wakijichimbia visiwani
Zanzibar.
Akizungumza
baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam,
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe alisema wanaondoka na wachezaji wote ambao
wamesajiliwa msimu huu.
“Tutaondoka
alfajiri na tutakwenda kuweka kambi Tukuyu lakini tutakwenda Mbozi kucheza na
Kimondo FC ambayo inacheza daraja la kwanza na tutacheza na timu ya Zesco ya
Zambia na Butter Bullet ya Malawi kwenye Uwanja wa Sokoine”, alisema Hafidh
Azam FC na
Yanga watamenyana Agosti 22, mwaka huu
katika mchezo wa Ngao, kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara
itakayoanza Septemba 22.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kukata na shoka
kutokana na upinzani wa Azam FC na Yanga katika miaka ya karibuni, zikiwa ndizo
timu ambazo zinapokezana ubingwa wa Ligi.
Ikumbukwe mara ya mwisho zilipokutana katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Kagame timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana kabla ya Azam FC kushinda kwa penalti 5-3 hivyo kwenye mechi ya ngao ya jamii iwapo timu hizo hazitafungana ndani ya dakika 90, mikwaju ya penalti itaamua mshindi.

No comments:
Post a Comment