JANA USIKU, ndani ya
Uwanja wa Nyumbani Nou Camp, Mabingwa wa Spain Barcelona wamefanikiwa kutwaa
Supercopa De Espana baada ya kutoka 0-0 na Atletico Madrid na wao kutwaa
Kombe hilo kwa vile walitoka sare 1-1 Wiki iliyopita huko Estadio Vicente
Calderon na hivyo kufuzu kwa Bao la Ugenini. Katika Mechi hiyo Kipa wa
Barca Victor Valdes alionyesha umahiri mkubwa kwa kuokoa Goli za wazi za Arda
Turan na David Villa. Atletico walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya
Filipe Luis kupewa Kadi Nyekundu na Mechi hii kwisha kwa Barca kupewa Penati ya
Dakika ya 89 kufuatia Pedro kuangushwa na Miranda na Lionel Messi akapiga na
Mpira kupiga posti. Akilalamikia Penati hiyo, Mchezaji wa Atletico Turan ambae
alikuwa tayari yupo Benchi baada ya kubadilishwa alipewa Kadi Nyekundu na
Refa.
Luis alipewa Kadi
Nyekundu kwa kumpiga Dani Alves katika Dakika ya 89. Neymar, ambae alianza Mechi
hii, alishindwa kushirikiana vyema na Messi. Hili ni Taji la 16 kwa Barca katika
Miaka minne na la kwanza kwa Kocha mpya Gerardo ‘Tata’ Martino ambae alisema
Taji hilo ni la Kocha aliemtangulia ambae ni Mgonjwa, Tito Vilanova. Alisema:
“Nimeshinda Taji hili kwa ajili ya mambo yalivyotokea. Kombe hili ni la
Wachezaji, Tito Vilanova na Wasaidizi wa Makocha!”
Mshindi: Bao la Neymar katika mechi ya kwanza limempa taji la kwanza Barcelona
Neymar (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake, Dani Alves na Super Cup ya Hispania
Mabingwa: Barcelona wamesherehekea rekodi ya kutwaa Super Cup ya 11 Hispania dhidi ya Atletico Madrid
Mchuano: Lionel Messi (kulia) akipambana na David Villa
Mkwaju wa penati
Juanfran wa Atletico Madrid (kushoto) akigombea mpira wa juu na Neymar wa Barcelona (kulia)
Anapaa: Cesc Fabregas akiwatoka Joao Miranda na Mario Suarez (kulia)
Mchezaji mwenzake wa zamani: Gerard Pique (kulia) akipambana na mshambuliaji wa Atletico, David Villa
Bao la wazi: Nyota wa Barcelona, Neymar akisikitika baada ya kukosa bao
Anavuta jezi: Arda Turan wa Atletico akimvuta jezi Messi

Barcelona
|
Atlético
Madrid
| |
Possession
|
78%
|
22%
|
Total
Shots
|
8
|
8
|
Shots on
Target
|
1
|
3
|
Pass
Accuracy
|
90%
|
69%
|
Fouls
|
9
|
27
|
Offsides
|
0
|
2
|
Yellow
Cards
|
3
|
3
|
Red
Cards
|
0
|
2
|
No comments:
Post a Comment