-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Coastal
Union iliyochezwa jana (Agosti 28 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 152,296,000. Watazamaji 26,137 walikata tiketi kushuhudia
mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 23,231,593.22.
Mgawo mwingine ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 18,786,827.52, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi
sh. 11,272,096.51, Kamati ya Ligi sh. 11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 4,383,593.09
No comments:
Post a Comment