Liverpool walipelekwa Dakika 120 kwenye Mechi ya Raundi
ya Pili ya Kombe la Ligi, CAPITAL ONE CUP, walipocheza na Timu iliyo Daraja la
3, Ligi 1, Notts County na kutoka Sare 2-2 katika Dakika 90 na hatimae kushinda
4-2 kwenye Dakika za Nyongeza 30 na kutinga Raundi ya Tatu.
Liverpool waliongoza 2-0 kwa Bao za Raheem
Sterling na Daniel Sturridge lakini Kipindi cha Pili Yoann Arquin na Adam
Coombes wakaisawazishia Notts County na Mechi kwisha 2-2 katika Dakika 90.
Katika Dakika za Nyongeza 30, Sturridhe na
Jordan Henderson wakaipa Liverpool Bao 2 na kushinda 4-2.
Timu nyingine za Ligi Kuu England ambazo
zilishinda Jana ni WBA, Sunderland, Southampton, Fulham [kwa Penati], Norwich,
Hull City na West Ham.
Crystal Palace ilibwagwa 2-1 na Bristol
City.
Katika Raundi ya Tatu, zile Timu za Ligi Kuu
England ambazo zinashiriki Mashindano ya UEFA Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI na
EUROPA LIGI, zitaanza kushiriki.
Raheem Sterling ndiye aliyeifungulia bao la kwanza
Liverpool
Sterling akiuvuta mpira
Aly Cissokho aliumia na kulazimika kutolewa nje
Kolo Toure hakujiweza ..alibebwa na stretcher na
kutolewa nje ...
Kapteni wa Gerard Liverpool akionesha alama ya vidole
ya 2-2 kwa maana ngoma bado mbichi
mchezaji Joss Labadie wa Notts County kwenye patashika
kugombea mpira jana usiku
Yoann Arquin akitupia kwa kichwa na mpira kugonga
posti
Adam Coombes akishangilia baada ya kusawazisha
Coombes (No 14) akipongezwa na wenzake na mpira kusonga
mbele kwa dakika 120
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet, Johnson, Toure, Wisdom,
Cissokho (Agger 10min), Gerrard, Allen (Henderson 65), Alberto (Countinho 72),
Ibe, Sturridge, Sterling. Subs not used: Brad Jones, Aspas, Lucas, Borini.
Booked: Wisdom, Sterling.
Goals: Sterling 4, Sturridge 29, 105, Henderson 110.
Notts County: Bialkowski, Dumbuya, Liddle, Smith, Stevens, Bell (Coombes 82), Labadie, Fotheringham (Boucaud 72), Campbell-Ryce (Thompson 71), Arquin, McGregor.
Subs not used: Murray, Spiess, Tempest, Nangle.
Booked: Campbell-Ryce, Arquin
Goals: Arquin 62, Coombes 84.
Attendance: 42,231.
No comments:
Post a Comment