Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu
gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘
kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Show.
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII
Nassib
Abdulmalick maarufu kama Diamond Platinum, ameonyesha yeye ni mkali na
mwenye fedha nyingi baada ya kukusanya watu kibao katika hoteli ya
Serena, Posta, jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa video yake ya My
Number One.
Msanii Diamond akiwa Serena Hoteli alipozindua video ya wimbo wake wa My Number One.
Mbali na uzinduzi huo, pia msanii
alitumia fursa hiyo kumkabidhi gari alilomnunulia mwanamuziki mkongwe
nchini, Muhidin Gurumo, aliyestaafu muziki, huku akisema hajafanikiwa
kununua hata baiskeli.
Diamond akimkabidhi mzee Muhidin Gurumo gari, ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza kustaafu muziki.
Katika
mazungumzo yake, Diamond alisema kuwa anathamini mchango wa wanamuziki
waliyotangulia, kwakuwa wao ndio waliyosababisha sanaa yao izidi
kuchanja mbuga.
"Namthamini
mno mzee Gurumo na wanamuziki wengine wote wa Tanzania, maana bila wao
sisi tusingeweza kusimama hapa tulipokuwa sasa, ukizingatia kuwa wao
ndio kila kitu," alisema Diamond.
Naye
mzee Gurumo alisema haamini macho yake baada ya kupewa ufunguo wa gari
lililonunuliwa na msanii Diamond, ambaye kwake ndio chaguo kwa waimbaji
wa Bongo Fleva,.
"Namshukuru
huyu kijana na Mungu ampe mafanikio makubwa zaidi katika tasnia ya
muziki wa kizazi kipya ili aendelee kuwa juu zaidi kwa kitendo chake
hiki ambacho kinashangaza wengi," alisema.
Diamond
ndio msanii wa kwanza kufanya kitendo cha kiungwana kama hicho, huku
pia mkutano wake ukifana kwa kualika wadau mbalimbali wenye majina yao
kwa ajili ya kushuhudia anachofanya ndani ya Hoteli ya Nyota tano ya
Serena, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment