BONDIA
wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka, leo anatarajia kumaliza ubishi na mpinzani
wake kutoka Marekani, Phil Williams, katika pambano la kuwania ubingwa wa
dunia.
Pambano
hilo la raundi 12 uzito wa kilogramu 76, litafanyika kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza
wakati wa kupima uzito, Cheka kutoka Morogoro alisema kuwa atamchapa Mmarekani ili kudhihirisha ubora
wake.
“Nimejiandaa
vya kutosha na matumaini yangu ni kuendeleza ubabe ili kubakisha mkanda huo
nyumbani,” alisema.
Alipoulizwa
kama anamjua mpinzani wake, Cheka alisema kuwa hajaona CD za mpinzani wake, ila
amejipanga kwa vita.
“Mimi
ni bora na nimejipanga vya kutosha, mpinzani wangu nitampiga raundi za mwanzo
mwanzo licha ya kutoona CD zake,” alisema Cheka.
Phil
Williams alisema ameona video za mpinzani wake na tayari amesoma mbinu
anazotumia akiwa kwenye mapambano.
Alisema
kuwa ameshinda mapambano 11 yote kwa TKO, hivyo na Cheka ajiandae kwa kichapo
hicho hicho.
“Sijawahi
kushinda kwa pointi, mapambano yangu yote kwa TKO, hivyo nimeshasoma mbinu za
Cheka ajiandae,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Rais wa WBF, Francois Botha, ambaye aliwahi kuwa bingwa wa
dunia wa uzito wa juu, alitoa kali ya
mwaka baada ya kuzigomea ‘gloves’ za waandaaji wa michuano hiyo na kusema kuwa
hazina viwango.
Alisema
kuwa ‘gloves’ hizo zimechakaa na hazina sifa za kuvaliwa kwenye pambano la
kimataifa kama hilo.
“Kwanza
zimechakaa halafu zipo chache, zinatakiwa gloves mpya nne kwa ajili ya pambano
hilo,” alisema.
Alisema
kuwa pambano hilo litakuwa na waamuzi wawili
kutoka Afrika Kusini na wawili Tanzania.
Aliwataja
waamuzi hao kuwa ni Darryl Rinnoiak, Edward Maeshall wa Afrika Kusini na Fedel
Hines, Goha Chagu wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment