Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 19, 2013

UTATA USAJILI WA NEYMAR

RIO DE JENEIRO, Brazil
MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Brazil na Santos, Neymer ni kati ya wachezaji ambao usajili wake msimu huu umetikisa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Usajili huo ulivitikisa vichwa vya mashabiki mbalimbali wa soka kutokana  na nyota huyo kuwindwa na timu mbalimbali kubwa barani Ulaya.
Hata hivyo kitendo cha  nyota, kujiunga na Barcelona ya Hispania, kimezua sintofahamu katika klabu ya Santos alikotokea.
Moja ya wahisani wa Neymar, Kampuni ya  Supermarket 'DIS' nchini humo inaamini nyota huyo alistahili kuuzwa kitita kikubwa cha fedha zaidi ya euro milioni 57 walizoopewa.
Licha ya uhamisho huo, DIS inayomiliki asilimia 40 kwa kinda huyo,imesema haijapewa 'kilicho chao' katika uhamisho wa kinda huyo na kutishia kuchukua hatua za kisheria ili kupata haki yao.
Kiongozi wa kampuni hiyo, Idi Sonda, hivi karibuni aliilalamikia Santos kukubali ofa hiyo, wakati awali walikubaliana Barca kuongeza dau.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa DIS Roberto Moreno, amewataka kuufunga mjadala kuhusu uhamisho wa Neymar (21) na kuahidi kuchukua hatua za kisheria itakapobidi.
Kasheshe hiyo, imechochewa na tetesi zilizozagaa, kwamba Santos italipwa kiasi cha euro mil.2, endapo mchezaji huyo ataingia kwenye orodha ya wachezaji watatu watakao wania tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or msimu huu.
Santos, itaingiza kibindoni mapato yatakayopatikana kwenye mchezo wa kirafiki uliopagwa na timu zote , huku Barca wakilazimika kulipa euro mil. 4.5 endapo mechi hiyo haitafanyika.
Inaonekana Santos wanataka kupiga dili hilo kimya kimya, ikiwa mpaka sasa DIS hawajapewa taarifa hizo. Hali ilizua vurumai baina ya wawili hao.

Moreno, amebainisha mpaka sasa DIS, haikupokea hati (dokumenti) yoyote ya uhamisho wa Neymar.
“Sijawahi kuoneshwa hati hata moja, nataka niwafuate Santos, halafu ndipo nitaamua kama tutakwenda mahakamani ama la!,” Moreno alisema.
Tovuti moja nchini humo, juzi ilitoa taarifa kampuni hiyo kuwa kwenye mipango ya kulifikisha suala hilo mahakamani.
Mwezi uliopita, Moreno aliwatishia klabu zote Santos na Barcelona, na kutoa onyo kali kwa kuwapa wiki moja kabla ya kufungua shitaka kutaka kujua mpango walionao Santos".

DIS, waligharimikia euro mil 2.6 katika usajili wake 2009, ambapo kujiunga kwake na mabingwa wa Hispania, wangeingiza euro mil.6.8 kutokana na asilimia 40 wanazo miliki.

Santos, ilipata faida ya euro mil.17 huku euro mil.40 zilikwenda sehemu nyingine ikiwemo familia ya mchezaji  huyo.

No comments:

Post a Comment