Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 19, 2013

MAKINDA WATAKAOMBEBA MOURHINO

LONDON, England
KOCHA , Jose Mourinho amewasili tena kuinoa  Chelsea ikiwa ni mara ya pili baada ya kuondoka katika timu hiyo miaka kadhaa iliyopita.

Kocha huyo ambaye ametokea kwenye timu ya Real Madrid safari hii atakutana na  timu yenye vijana wengi na wenye vipaji ambao mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovich amewanunua baada ya kushindwa kuinua vipaji vya vijana katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa sasa timu hiyo ina wachezaji chipukizi kama vile, Nathan Chalobah, Nathan Ake, Jamal Blackman  na  Lucas Piazon ambao wanatajwa kuwa huenda wakawa wachezaji muhimu katika timu hiyo, ingawa wamekuwa hawatumiki.

Mbali na hao pia wapo wengine kama  Oscar, Hazard na Azpilicueta ambao msimu uliopita waliweza kuonesha uwezo wao.

Pia wakati   Courtois akikipiga kwa mkopo katika timu ya  Atletico Madrid  katika makala haya tunaangalia chipukizi wengine ambao mashabiki wa  Chelsea wanatarajia msimu huu  huenda wakambeba  Kocha Jose Mourinho endapo atawatumia.

1.    Marco van Ginkel
Kinda huyo ambaye anacheza nafasi ya kiungo mkabaji tayari ameshafikia uwezo wa kuchezea timu ya Taifa ya Uholanzi.

Akiwa na mwenzake  Louis van Gaal, kinda huyo  ndiye aliyeiwezesha timu ya vijana  ya Uholanzi wenye umri chini ya miaka 21 kutwaa ubingwa wa Ulaya.

Inaelezwa kwamba kutokana na nguvu  na kasi yake ndivyo vitakavyomuwezesha kupata namba katika kikosi cha Mourinho.

Mbali na hilo pia inaelezwa kuwa kutokana na kuwa Essien hayupo fiti na huku  Oriol Romeu akiwa amepelekwa kwa mkopo jambo hilo linaweza kumfanya Mholanzi huyo kupata nafasi ya kuonesha uwezo wake msimu huu.

2.      Andre Schurrle
Kinda huyo Mjerumani ambaye anakipiga pia kwenye timu ya taifa amesajiliwa msimu huu kwa pauni milioni 18 akitokea timu ya  Bayer Leverkusen.

Hadi sasa mshambuliaji huyo wa pembeni ameshachezea timu ya Taifa ya Ujerumani mara  24 licha ya kuwa na umri mdogo jambo ambalo linadaiwa linaweza kumsaidia kama ilivyokuwa kwa  mwenzake, Marko Marin.
Inaelezwa kuwa kinda huyo anaweza kucheza kama mshambuliaji wa pembeni ama kama mshambuliaji wa kati jambo ambalo linadaiwa  Mourinho anaweza kumtumia mara kwa mara kulingana na mechi.

Kinda huyo nyota anadaiwa kuwa na kasi na mwenye mashuti ya nguvu jambo ambalo litamfanya  kuwa hazina kwa kocha huyo.

3.    Romelu Lukaku
Raia  huyo wa  Ubeligji aliutumia msimu uliopita akikipiga katika  timu ya  West Brom, ambako alifanikiwa kufunga mabao  17 katika mechi alizoichezea timu hiyo kwenye mashindano yote.
Msimu uliopita ndiyo wa kwanza kwa nyota huyo kucheza  kwenye Ligi Kuu ya  England baada ya kusugua benchi kwa muda mrefu ndani ya klabu hiyo.

Kutokana na nguvu na umbile lake ambalo limewafanya mashabiki wa timu hiyo kumpachika jina la  Drogba mpya inasemekana  Mourinho atamtumia mshambuliaji huyo kutokana na kwamba  ndiyo wachezaji wa aina hiyo anaowapenda.

Inaelezwa kuwa licha ya  Chelsea kuwa bado inahitaji kusajili washambuliaji wapya ingawa inao wengine kama kinda huyo Mbelgiji, Torres na  Demba Ba, lakini itamlazimu,  Mourinho  kumtumia mshambuliaji mwenye nguvu ili aweze kumaliza msimu huu bila kuchanganyikiwa.
 
4.    Kevin De Bruyne
Huyo pia ni mshambuliaji mwingingine raia wa Ubelgji ambaye aliutumia msimu uliopita akikipiga kwa mkopo ambaye anatajwa pia msimu huu anaweza kumbeba  Mourinho.

Baada ya kuitumikia timu ya  Werder Bremen  na kufanikiwa kufunga mabao 10 na kusaidia kupatikana mengine  10 nyota huyo anaonekana kuwa ataweza kusimama vilivyo katika nafasi ya mshambuliaji wa pembeni.

Inaelezwa kuwa kutokana na uwezo aliounesha wa kuwasumbua wapinzani wake nyota huyo anaweza pia kufanya  hivyo msimu huu akiwa na Chelsea.


Kutokana  na kasi yake na uwezo wa kumliki mpira, De Bruyne anaweza kuifanya Chelsea kuwa tishio msimu ujao.

No comments:

Post a Comment