Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 19, 2013

MANCHESTER CITY YACHAPWA NA AMAZULU FC BILA KOCHA WAO PELLEGRINI ALIETIMKA KWAO CHILE

Kikosi cha Man City na Amazulu Fc wakijipanga kabla ya mtanange kuanza.CITY, wakicheza bila ya kuwa na Meneja wao mpya Manuel Pellegrini, wamepokea kipigo chao cha pili mfululizo huko Nchini South Africa baada ya Usiku huu kufungwa na AmaZulu Bao 2-1 katika Mechi ya Kirafiki ya Mwaliko unaoitwa ‘Nelson Mandela Football Invitational’ iliyochezwa ndani ya Moses Mabhida Stadium Mjini Durban.


Man City walicheza Mechi hii chini ya Meneja Msaidizi Brian Kidd baada ya Meneja wao mpya, Manuel Pellegrini, kupata udhuru wa Kifamilia na kurudi haraka kwao Chile.

Bao la ushindi kwa AmaZulu lilifungwa kwa Penati ya Carlington Nyadombo katika Dakika ya 89.

Jumapili iliyopita, Man City ilichapwa Bao 2-0 na Klabu nyingine ya South Africa, SuperSport, United kwenye Mechi iliyochezwa huko Pretoria.
Man City sasa wanasafiri kuelekea huko Hong Kong ambako Jumatano ijayo watacheza na South China.


Mashabiki wa Africa wakionesha sapoti zao kwa timu ya City!!


Kapten wa City Vincent Kompany akigusa mpira
Edin Dzekoakiimarisha ...wakicheza na AmaZulu
VIKOSI:
AmaZulu: Kapini; Macala, Teyise, Msekeli, Hlanti; Madondo, Madubanya, Manqana, Zondi, Dlamini; Ndulula.
Subs: Mathibe, Zikalala, Mwedihanga, Nyadombo, Van Heerden, Cele, Issah, Mthiyane, Nsele, Manoka, Dlamini, Ngcobo.
Goals: Ndulula 20, Van Heerden pen 87
Man City: Hart (Pantilimon 63); Richards (Zabaleta 46), Kompany (Garcia 46), Nastasic (Lescott 69), Kolarov; (Boyata 75) Milner (Razak 75), Toure (Rodwell 46), Fernandinho (Barry 69), Sinclair; Dzeko (Nimely 75), Nasri (Suarez 69).
Subs not used: Huws.
Goal: Milner 26

MANCHESTER CITY-ZIARA:
May 24 Chelsea (Busch Stadium, St Louis) =USHINDI 4-3
May 25 Chelsea (Yankee Stadium, New York) =USHINDI 5-3
Julai 14 Supersport (Loftus Versfeld) =KIPIGO 2-0
Julai 18 AmaZulu (Moses Mabhida Stadium, Durban) =KIPIGO 2-1
Julai 24 South China (Hong Kong Stadium, Hong Kong - Barclays Asia Trophy) SAA 9 NA NUSU MCHANA
Julai 27 Tottenham/Sunderland (Hong Kong Stadium, Hong Kong - Barclays Asia Trophy) KUJULISHWA
Julai 31 AC Milan (Allianz Arena, Munich - Audi Cup) SAA 1 NA ROBO USIKU
Agosti 1 Bayern Munich/Sao Paulo (Allianz Arena, Munich - Audi Cup) 
Agosti 10 Arsenal (Olympic Stadium, Helsinki) SAA 11 JIONI

No comments:

Post a Comment