Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 19, 2013

WAKALI 8 WALIOTIKISA UHAMISHO LA LIGA HADI SASA

MADRID, Hispania
WAKATI  mchakato wa   usajili ukizidi kupamba moto Ulaya, baadhi ya Ligi zimeonekana kulitilia maanani sakata hili. Ligi Kuu Hispania, ni moja ya Ligi zilionesha nia ya kuvalia njuga usajili, huku kukiwa na idadi kubwa ya nyota kusaini na wengine kuondoka.
Tayari timu zimemwaga mamilioni kuvinoa vikosi vyao kabla ya kuanza kwa msimu mpya, ingawa muda unaruhusu kuleta vifaa na kutoa mizigo.
Makala haya yameangazia, nyota nane ambao mpaka sasa wametishia katika uhamisho huu. Wakiajiliwa na wengine kuondoka.
 

Radamel Garcia Falcao

Anabaki kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa kikita kikubwa msimu huu, baada ya kusaini Monaco ya Ufaransa akitokea Atletico Madrid ya Hispania kwa ada ya euro mil.60.
Falcao "El Tigre" alikuwa akiwindwa na vigogo kadhaa Ulaya, lakini aliacha gumzo baada ya kukubali ofa ya timu iliyopanda daraja msimu huu.
Alikuwa na kila kigezo cha kuchezea timu yoyote ile hapa duniani, kutokana na kiwango alichoonesha tangu atue Atletico Madrid, huku akifunga mabao 52 katika michezo 67 msimu uliopita.
 

Neymar da Silva Junior

Wakati kinda huyp wa Brazili aliposaini Barcelona, mwanzoni mwa  mwezi Juni, mabeki wa timu pinzani,  hazitia wasiwasi ujio wake.
Neymar alijiunga na Barca kwa ada ya euro mil.57 akitokea Santos ya Brazil, lakini alianza kuzitia hofu timu pinzania baada ya kuonesha maajabu kwenye michuano ya Kombe la mabara lililofanyika Brazil. Aliongoza nchi yake kutwaa kombe huku yeye akiibuka mchezaji bora wa michuano. Amekwenda Camp Nou anakutana na mchawi wa soka duniani, Lionel Messi, lazima wakae.
“Ilikuwa ndoto yangu muda mrefu kutua Nou Camp. Na leo ndoto imetimia. Sikuwahi kufikiria kuja hapa kwa nia ya kuwa mchezaji bora, kama ni mchezaji bora yuko hapa- Messi” alisema Neymar wakati akitambulishwa Camp Nou.

Isco

Francisco Roman Suarez ‘Isco’, amejiunga na Real Madrid kwa kiasi cha euro mil.30 akitokea Malaga ya nchini humo pia.
Ni miongoni mwa Yosso walio kwenye kiwango cha juu kwa sasa nchini Hispania, na hii ni kutokana na mafanikio yake ya kuifuikisha Malaga robo fainali kwenye michuano ya Uefa, ikiwa ni ni mara ya kwanza kwa timu hiyo.
Lakini amezua utata, baada ya kumdharirisha Lionel Messi kwa kumfananisha na mbwa.
“Nilimwita mbwa wangu jina la Messi, sababu Messi ni mchezaji bora wa dunia,hivyo Messi ni mbwa wangu”, lilipoti gazeti la Metro.
 

Jesus Navas

Winga huyo ametua Manchester City ya England akitokea klabu ya Sevilla kwa ada ya uhamisho wa euro mil.17.5 Juni.

Uhamisho wake ulikuwa gumzo kote, kutokana na imani ya wachezaji wa Kihispania kupenda kucheza nyumbani.
City, hupendelea soka la kizamani kumuona mchezaji anakaba na kufunga mara zote, ila Navas sio mtu wa namna hiyo, kwani alishindwa kuthibitisha hilo akiwa Sevilla. 

Benat Etxebarria

Benat ameamua kuirudia timu yake ya zamani Athletic Bilbao, baada ya kukubaliana na Real Betis kwenda kwa euro mil.8.
Mkataba wa miaka mitano aliyposainisha umezivunja moya timu za West Ham na Bolton za England zilizokuwa zikinyemelea saini yake.
Kiungo huyo ‘aliweka ngumu’ kusaini tena Betis, hali iliyowafanya kumuuza kuliko kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao.

Dani Carvajal

Amejikuta akirejea nyumbani Santiago Bernabeu, baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka kadhaa akiwa Bayern Leverkusen. Ni zao la akademi ya Madrid, kabla ya kujisafishia nyota na kuitwa timu ya kwanza muda mfupi.
Msimu mmoja baadae. Madrid walimuuza kwa euro mil.5, lakini wamelazimika kumrejesha kwa euro mil.6.5 kutokana na kiwango chake kupanda kwa kasi.

Leo Baptistao

Atletico Madrid wanasubiria ahadi aliyotoa nyota  huyo raia wa Brazil. Safari yake kutoka Rayo Vallecano kwenda Atletico, hata kwa mguu angetembea. Ni majirani sana.
Amesainishwa kwa uhamisho wa euro mil.7, baada ya kuichezea Vallecano mechi 28 tu msimu uliopita.
“Nina furaha kubwa kurejea kwetu. Naahidi kujitolewa kwa lolote Atletico na kujifunza mengi . Bado mie ni kijana mdogo, miaka 20,”
 
David Villa
Anaungana na Baptistao Atletico Madrid  katika mbio za kuwinda ubingwa wa La Liga. Villa anakuwa mbadala wa Falcao aliyetimkia Monaco kwa ada ya uhamisho wa euro mil.5 akitokea Barcelona.
Nyota huyo (31), alisaini Barca 2011, akitokea Valencia, lakini ameshindwa kwendana na kasi ya Wana-Catalunya hivyo kupigwa benchi mechi nyingi.
Bado vuguvugu linaendelea, huenda mastaa kuongezeka ama kupungua La Liga


No comments:

Post a Comment