Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akiongea na waandishi |
Hapa wakuu wanateta jambo |
Timu ya Airtel Rising Stars ikiwa na uongozi wa soka pamoja na Kampuni ya Airtel |
Timu ya Airtel Rising stars iliyopita |
Waandishi wa habari |
MASHINDANO ya vijana ya Airtel Rising Stars yanatarajia kuanza
kutimua vumbi June mwaka huu katika viwanja tofauti.
Mashindano hayo ambayo ni msimu wa tatu kufanyika nchini yana
lengo la kukuza vipaji vya vijana.
Akizungumza jijini, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
Msanifu Kondo alisema kuwa michuano ya mwaka huu yatashirikisha mikoa sita
nchini.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ilala,
Temeke na Kinondoni ambapo watashiriki wanaume tu.
Alisema kuwa mikoa ya Tanga, Geita na Ruvuma itashirikisha wanawake
ambao itakuwa kwa mara ya kwanza kushiriki.
“Tumepania kuboresha mashindano ya mwaka huu ndio mana kuna
mikoa mpya ambayo imeongezwa ila kupata vipaji vipya,”alisema.
Nae Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano alisema kuwa kwa mwaka huu wameungana na
kampuni ya Sumsung ila kuboresha michuano hiyo.
“Watu wajiandae na wakae tayari kwa ajili ya changamoto na
kuinua vipaji vya mchezo huu nchini,”alisema
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa
Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo aliitaka kampuni hiyo kuanzisha klinki maalum
itakayoweza kuboresha vipaji vya vijana nchini.
No comments:
Post a Comment