MABINGWA watetezi wa Mkoa wa Kilimanjaro wa mashindano ya Pool,Chuo kikuu cha MUCCOBS, juzi walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani Kilimanjaro yajulikanayo kama 'Safari Lager Higher Learning Competition 2013' baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Chuo kikuu cha MWENGE yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mambuo mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yaliyoshirikisha vyuo
vikuu vinne vya mkoani hapo ambavyo ni MUCCOBS, MWENGE, KCMC na SMMUCO kwa
udhamini wa Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari
Lager.
Chuo cha MUCCOBS kwa kutetea
ubingwa huo kilijinyakulia fedha taslimu Sh.500,000 pamoja tiketi ya
kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro katika fainali za taifa zinazotarajiwa
kufanyika Juni mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na chuo cha
MWENGE ambacho kilijinyakulia kitita cha Sh.300,000.Nafasi ya tatu ilichukuliwa
na chuo cha KCMC ambacho kilizawadiwa Sh.200,000 na nafasi ya nne ni Chuo cha SMMUCO
ambacho kilipata Sh.100,000.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja
(wanaume), Idrisa Juma wa KCMC aliibuka kuwa bingwa hivyo kujinyakulia pesa
taslimu Sh.150,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwa upande wa wachezaji
mmoja mmoja.Nafasi ya pili ilichukuliwa na Kim Kunthea wa KCMC ambaye
alizawadiwa Sh.100,000.
Na kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja
(wanawake), Winfrida Mponzi wa MUCCOBS alitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa pesa
taslim sh.100,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika mashindano ya
kitaifa.Nafasi ya pili ilichukuliwa na Aluiya Herode wa chuo cha SMMUCO ambaye
alizawadiwa pesa taslim Sh 50,000.
Wakati jijini Arusha Mabingwa watetezi,
IAA walifanikiwa kutetea ubingwa wao wa Mkoa dhidi ya Chuo cha SILA, na kwa
nafasi hiyo IAA ilijinyakulia kitita cha Shilingi 500,000 pamoja na tiketi ya
kushiliki mashindano ya kitaifa . huku nafasi ya pili ikishikiliwa na SILA ambao walijinyakulia kitita cha Shilingi
300,000.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na CDTI
ambao walizawadiwa pesa taslimu sh.200,000.
Upande wa wachezaji mmoja mmoja wanaume
Bingwa mtetezi wa Mkoa,Baraka Shayo alitetea ubingwa wake dhidi ya Baraka
Robert wa chuo cha SILA, na kwa ubingwa huo, Baraka alijinyakulia pesa taslimu
sh.150,000/= na nafasi ya pili ilichukuliwa na Baraka Robert wa SSILA am
No comments:
Post a Comment