Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.
Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.
Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa wakipotosha jamii.
No comments:
Post a Comment