Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 14, 2013

SIMBA YATOKA SARE YA 2-2 NA AZAM TAIFA LEO

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza



John David wa Azam na Haruna Chanongo wa Simba wakiwa wameangukiana 

Mshambulia wa Azam, Himid Mao akiondoka na mpira huku Haruna Chanongo akimwangalia

John David wa Azam akiokoa mpira kwenye eneo la hatari huku Haruna Chanongo akifikiria jinsi ya kumnyanganya
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao kwa staili ya aina yao
Mwadini Ally akiwa amedaka mpira 


TIMU ya Azam FC leo imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu, Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo haya Azam imefikisha pointi 47, ikibaki nafasi ya pili, nyuma ya Yanga yenye pointi 52, huku Simba ikibaki nafasi ya nne kwa pointi zake 36.

Mabao ya Simba yalifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ aliunganishia nyavuni mara zote mbili dakika ya 10 na 14 pasi za Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kushoto.

Kipre Tchetche aliifungia Azam kwa penalti dakika ya 29, baada ya Khamis Mcha kuangushwa kwenye eneo la hatari na William Lucian.

Mwamuzi  Oden Mbaga alimwondoa kwenye benchi kocha Muingereza wa Azam, Stewart Hall dakika ya 31 baada ya kulalamikia uchezeshaji wa refa huyo.
Kipindi cha pili, Azam walirejea kwa nguvu kusaka bao la kusawazisha na wakafanikiwa dakika ya 72 baada ya Humphrey Mieno kuunganisha shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na kiungo Khamis Mcha.
Baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu na mara kadhaa timu zote mbili zilikosa mabao.

Kikosi cha  Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Mussa Mudde, Shomari Kapombe, Amri Kiemba, Haroun Chanongo/Edward Christopher, Abdallah Seseme, William Lucian/Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Singano na Mrisho Ngassa/Fliex Sunzu.

Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Luckson Kakolaki/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk, Salum Abubakar, John Bocco/Abdi Kassim, Humphrey Mieno/Jabir Aziz na Kipre Tchetche.

 Katika hali ya kushangaza mashabiki wa Yanga walikuwa wakishangilia timu ya Simba kitu ambacho ni nadra sana kukiona kwenye mechi zinazohusisha moja ya timu hizi.

No comments:

Post a Comment