Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, April 13, 2013

KIPRE TCHETCHE: SIMBA HAITOKI LEO TAIFA

MCHEZAJI wa Azam FC,Kipre Tchetche ametamba kuimaliza Simba katika mchezo wa leo,hata kama timu hiyo ina wachezaji vijana.
Akizungumza na Lenzi ya Michezo alisema Simba hawawezi kuwashinda, tena kipindi hichi ambacho kikosi kizima kina wachezaji vijana,ambao bado  hawajaizoea Ligi vizuri .

Mchezaji huyo alisema ,matamanio yake ni kuisaidia timu yake iweze kuwa bingwa wa ligi msimu huu, kwani hayo ni malengo ya wachezaji na kocha wao Stewart Hall.
“Mazoezi tumefanya,tumejipanga kuhakikisha Simba hawapati nafasi ya kupunguza machungu yao, badala yake tutaendeleza kipigo kwa kwenda mbele,” alisema Tchetche
Alisema ushirikiano ambao umejengeka baina ya wachezaji wa timu hiyo,umeonyesha mwamko wa kushinda, hivyo Simba wasitarajie mteremko na kujipa matumaini ya kushinda mechi hiyo.
                                                                                   

No comments:

Post a Comment