Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 14, 2013

MOURINHO AIFANYIA USHUSHU BORUSSIA DORTMUND IKIIFUNGA GREUTHER FURTH MABAO 6-1

Amon the crowd in the Trolli Arena was Real Madrid coach Jose Mourinho, whose side face Dortmund in the Champions League semi finals later this monthBorussia Dortmund have thrashed the Bundesliga’s bottom club Greuther Fürth 6-1 at the Trolli Arena


Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho ameonyesha yuko makini na kazi yake baada ya kuvamia katika mechi ya Borussia Dortmund kimyakimya. 
Mourinho raia wa Ureno, alikuwa kati ya watazamaji wakati ikiichapa Furth kwa mabao 6-1. 
Dortmund imepangiwa kuivaa Real Madrid katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, moja ya mechi inayotabiriwa kuwa ngumu kwa timu zote. 
Timu hiyo ya Ujerumani ni kati ya timu ambazo zimekuwa zikiipa wakati mgumu Madrid kila zinapokutana. 
Mourinho alikuwa mtulivu jukwaani na mara kadhaa, picha za TV ya uwanjani zilikuwa zikimuonyesha na mashabiki walizomea kwa nguvu. 

Katika mechi hiyo, Dortmund waliovuka hadi nusu fainali kwa kuitoa Malaga walifanya mabadiliko manne kwa kutowatumia wachezaji ambao walicheza dhidi ya Malaga ya Hispania.
Marco Reus alikuwa na matatizo ya misuri, Marcel Schmelzer, Neven Subotic na Sven Bender walipumzishwa kutokana na kucheza mfululizo.
Mourinho amepania kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa pamoja na kutwaa kombe kabla hajaondoka Madrid.

No comments:

Post a Comment