Mwenyekiti wa Mkutano wa dharura wa klabu ya Simba, Mohamed Wande akifafanua jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Starlight jijini Dar es Salaam jana na kumg’oa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutanohuo, Bi. Chuma Suleiman ‘Hindu’ na Katibu wa Mkutano huo, Mohamrd said. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mzee wa Simba, Ally Mselemu akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwanachama wa Simba Saidi Mkumba cheche.
Mwanachama wa Simba, sofia Lubuva akitoa nondo zake za kumtaka Rage kung'oka madarakani.
Picha za wanachama wa Simba waliondoa uongozi madarakani
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment