KOCHA Mkuu wa Toto African, John Tegete amejigamba kuwa Simba wasitarajie mchelea kwenye mchezo wao wa kesho utakaochezwa uwanja wa Taifa.
Tegete ambaye yupo jijini tayari kwa mpambano huo amesema kuwa pamoja na kuwa Simba ni mwenyeji wa mchezo huo katu hawataweza kuwafunga kirahisi.
"Pamoja na kuwa Simba ni wenyeji wa mchezo wa kesho (leo) wasitegemee wataweza kutufunga kirahisi maana timu yangu ipo vizuri na wanaijua Simba", alisema Tegete.
Pia alisema Simba ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri lakini siyo kigezo cha kuwa wataweza kuwafunga kwani hata wao ni wazuri pia.
Toto African ni moja ya timu ambayo inacheza kiushindani kila inapokutana na Simba na kwenye mzunguko wa pili wa msimu uliopita walitoka sare.
Simba na Toto zinacheza mchezo wa kufunga pazia kwa mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2012/2013 wa ligi kuu ya Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment