Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 9, 2012

KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF YATOA TAREHE YA UCHAGUZI WA TABORA NA CHAMA CHA MAKOCHA

KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini limesema Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA) na Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Desemba 22 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba za uchaguzi za vyama hivyo, Kamati za uchaguzi zitatangaza mchakato wa uchaguzi Novemba 10 mwaka na fomu kwa wagombea uongozi zitaanza kutolewa Novemba 12 mwaka huu. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Novemba 16 mwaka huu.

Vileveile Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoa mwongozo huo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA baada ya kuomba hivyo kutokana na wagombea sita tu kujitokeza kuomba nafasi tatu za uongozi katika mchakato wa awali.

Wakati huohuo Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu.

Viongozi waliochaguliwa kuongoza MZFA ni Patrick Songora, Mwenyekiti, Nassoro Mabrouk, Katibu Mkuu na Richard Kadutu ambaye ni Mwakilishi wa vilabu TFF

Taarifa hiyo inasema ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MZFA walivyo na imani kubwa katika kusimamia mchezo huo katika Mkoa wa Mwanza.

TFF inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati za Utendaji ya MZFA iliyochaguliwa chini ya uenyekiti wa Patrick Songora aliyechaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo.
 
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya MZFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

.

No comments:

Post a Comment