Mshambuliajiwa timu ya Taifa ya Vijana U-17, Kelvin Manyika (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Ashanti United, Khan Usimba katika mechi ya kirafiki uliochezwa uwanja wa Karume jana |
TIMU ya vijana U-17 Serengeti boys jana uliifunga timu ya Ashanti United 2-0, mchezo uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es salaam
Ashanti ambayo ipo daraja la kwanza ilichezewa dakika zote 90 na ilipokea kipigo hicho dk ya tatu kupitia kwa mfungaji Mohamed Salum ambaye aliwapita mabeki na kuingia ndani ya eneo la goli na kuzamisha mpira wavuni.
Kipindi cha pili Serengeti boys waliwashtukiza Ashanti dk 52 na kujifunga wakati wakiokoa shuti la Miza Christopher.
Serengeti ambayo wapo kambini wakijiandaa na mchezo wa raundi ya pili ya kutafuta kufuzu fainali za vijana itacheza mchezo wao na Misri Octoba 14 jijini Dar es salaam.
Naye kocha msaidizi wa Serengeti boys Jamhuri Kiwelu "Julio" alisema timu yake ipo vizuri kupambana na Misri na anawashukuru wadau wote na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuiweka kambini timu muda mrefu kwani wachezaji wamezoeana vizuri.
"Ninawashukuru wadau na TFF kwa kuiwezesha timu kuweka kambi muda mrefu kwani imesaidia vijana kuzoeana na kucheza kwa kombinesheni nzuri", alisema Julio
Kocha wa Ashanti Mubaraka Hassan amesema anashukuru timu yake kupata mechi nzuri na ngumu kwani inawasaidia kurekebisha timu nafasi zinazoonekana zina mapungufu.
"Nashukuru kupata mechi ngumu na nzuri kwani inasaidia kuirekebisha timu, matokeo ya uwanjani ni changamoto kwangu"
Ashanti ni mara ya pili kwa kipindi kisichozidi miezi miwili kucheza na Serengeti boys na imefungwa mara zote.
No comments:
Post a Comment