Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 27, 2012

KAZI YAANZA REDD'S MISS TANZANIA 2012

Mashindano ya Redds Miss Tanzania yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo nayo imekamilika na kufanikiwa kuwapata warembo jumla ya 30.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa

Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.

Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.

Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).

Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.

Kwa kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao. 2013. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kushoto ni Meneja wa Kinywaji wa Redds Victoria Kimaro

No comments:

Post a Comment