MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS DKT. MWINYI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi
amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 26 Novemba 2026, katika
Ikulu ya Zanzibar.
Makamu wa Rais Mhe. Ndejembi amempongeza Rais Dkt.
Mwinyi kwa kazi anazoendelea kuzifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa
Zanzibar katika sekta mbalimbali, ikiwemo kushughulikia masuala ya Muungano na
utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitaifa.
Amesema mahusiano ya Tanzania Bara na Zanzibar yana
mizizi ya kihistoria na kindugu inayodhihirishwa na mwingiliano wa wananchi
katika biashara, familia, shughuli za kiuchumi na mahusiano ya kijamii.
Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Muungano wa Tanzania
umeendelea kuwa msingi muhimu wa kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya
serikali mbili katika kutatua changamoto na kusukuma mbele masuala yenye
maslahi kwa wananchi.

Post a Comment