DC Mpogolo Awapongeza Walimu kwa Kazi Kubwa ya Kuandaa Viongozi
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya katika jamii, akisema ni nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa kwa kuwa wanazalisha wataalamu na viongozi mbalimbali nchini.
Akizungumza katika sherehe za walimu za Kata ya Ukonga, 'Ukonga Day' jijini Dar es Salaam, Mpogolo alieleza kuwa walimu ni miongoni mwa watu wasio na wivu katika jamii kwani hufurahia kuona wanafunzi waliowafundisha wakifanikiwa na kuchukulia mafanikio hayo kama sehemu ya mafanikio yao wenyewe, huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya taifa.
Mpogolo amesema, walimu wamekuwa nyenzo muhimu katika kuwaandaa viongozi na wataalamu wanaochangia maendeleo ya taifa, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuthamini mchango wao.
Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga na mlezi wa walimu wa Kata ya Ukonga, Jerry Silaa, amesema mafanikio yake yamejengwa kwa kiasi kikubwa na walimu.
Silaa amesema alizaliwa katika Kata ya Ukonga na kusoma katika Shule ya Msingi Ukonga, hivyo anatambua na kuheshimu mchango mkubwa wa walimu wa kata hiyo katika safari yake ya mafanikio.

Post a Comment