DIPLOMASIA YA DK. SAMIA YAFUNGUA MILANGO YA AJIRA 50,000 JAPAN



Kukua kwa fursa za ajira kwa Watanzania katika nchi mbalimbali duniani kumetajwa kuwa ni matunda ya diplomasia makini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu amebainisha kuwa mahusiano mazuri ya kidiplomasia yameifanya Tanzania kuaminika, ambapo kwa sasa kuna fursa ya kukuza ujuzi nchini Japan kwa vijana 50,000. 

Vijana hao watakapokamilisha mafunzo yao, watatumika katika miradi mikubwa ya ujenzi ya Japan duniani kote, jambo ambalo litaongeza utaalamu na sifa ya Tanzania katika soko la ajira la kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa na serikali wakati wa kuwaaga vijana 109 wanaoenda kufanyakazi ughaibuni baada ya kupitia taratibu zote rasmi na kukamilkisha nmafunzio nya namna ya kwenda kuishi ughaibuni ikiwamo kufuata sheria za nchi hiyo.

Aidha Serikali imewahakikishia vijana wanaokwenda nje kuwa usalama na haki zao ni kipaumbele cha kwanza. Waziri Sangu ameeleza kuwa lipo dawati maalumu katika balozi mbalimbali linaloshughulikia changamoto za Watanzania hao, na serikali inatambua na kulinda kila raia aliyesajiliwa kupitia mifumo rasmi akiwa nje. Madawati hayo yamelenga kuondoa hofu na kuleta utulivu miongoni mwa vijana, huku serikali ikisimamia mikataba yao ili isivunjwe kiholela na kutekelezwa kwa haki.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala wa Ajira Tanzania Bara (TRAA), Abdallah Khalid Mohamed , ameipongeza serikali kwa kutengeneza mifumo inayolinda soko la ajira la nje. Tangu kuanzishwa kwa umoja huo mwaka 2020, wamefanikiwa kusaidia Watanzania wengi kupata kazi na kukabiliana na changamoto za ajira nchi za nje. 

Ushirikiano huu kati ya sekta binafsi na serikali umekuwa nguzo muhimu katika kupunguza tatizo la ajira nchini na kuimarisha ushindani wa nguvu kazi yetu kimataifa, amesema Mohamed.

Kwa kupitia mikakati hii, Serikali ya Awamu ya Sita inajenga msingi wa uchumi shindani ambapo Watanzania wanashiriki kikamilifu katika soko la ajira la dunia. Lengo ni kuhakikisha vijana wanakuwa na ujuzi (skills), nidhamu, na ulinzi wa kisheria wanapokuwa ughaibuni. 

Hii siyo tu inaleta utulivu wa kijamii kwa kutoa ajira, bali pia inaandaa nguvu kazi itakayokuja kuendeleza miradi mikubwa nchini Tanzania baada ya kupata uzoefu wa kimataifa.

No comments