MNYORORO WA NGOZI KIWANDA CHA KLICL KUZIMA KELELE ZA KUBAMBIKIZA ZA WACHOCHEZI



Yaliyopita yamepita Watanzania wanapaswa kuganga yajayo kwa kutumia raslimali zilizopo kujikwamua kiuchumi na kulikwamua taifa lao huku saikolojia ikiwa hapa ni kazi tu, kazi iendelee ikiambatana na kazi na utu tunasonmga mbele.

Wakati Tanzania inajenga misingi imara ya kiuchumi kupitia uwekezaji wa ndani unaogusa maisha ya mwananchi mmoja mmoja; uzalishaji wa bidhaa za ngozi nchini sasa umekuwa silaha ya kimkakati ya kuimarisha Shilingi yetu, kwani badala ya kupoteza fedha za kigeni kuagiza viatu na mikanda kutoka nje, tunazalisha wenyewe kupitia ubia wa kimkakati kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza. 

Hii ndiyo siri ya mafanikio ya sera za fedha: kuwa na uchumi unaozalisha bidhaa halisi zinazokidhi soko la ndani na ushindani wa kimataifa.

Vijana wa Kitanzania sasa wana fursa adhimu ya kufaidika katika mnyororo mzima wa thamani wa bidhaa za ngozi kuanzia ngazi ya vijijini hadi mijini. Mnyororo huu unaanzia kwa wafugaji, ambapo vijana wanaweza kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya utunzaji wa mifugo ili kupata ngozi bora isiyo na makovu, jambo ambalo huongeza thamani ya mifugo yao mara dufu. 

Katika hatua ya pili, viwanda vidogo vya kusindika na kutengeneza vifaa vya ngozi vinatoa nafasi kwa vijana wenye ubunifu kuingia katika soko la "staili" kwa kutengeneza bidhaa za kipekee kama mikoba, mapochi,viatu  na mavazi yanayovutia soko la kisasa kama majaketi.

Katika ngazi ya matumizi na soko, kiwanda cha KLICL Kilimanjaro kinatengeneza fursa nyingi za ajira kwa vijana kupitia usambazaji na uuzaji wa bidhaa hizo zenye viwango vya kimataifa. 

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeweka wazi kuwa upanuzi wa viwanda hivi unalenga kuongeza uzalishaji, jambo ambalo ni habari njema kwa wajasiriamali wadogo wanaoweza kuwa mawakala au wabunifu wa bidhaa ndogo ndogo zinazotokana na ngozi ya viwandani. Hii inatengeneza uchumi shindani ambapo kijana hahitaji kusubiri kuajiriwa ofisini, bali anaweza kuwa sehemu ya mnyororo huu unaozalisha faida kuanzia zizini hadi dukani.

Bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini sasa zina uwezo wa kushindana katika masoko ya kimataifa, jambo linalotupa uhakika wa kupata fedha za kigeni badala ya kuzipoteza. 

Hii ndiyo maana halisi ya uchumi wa viwanda: kuchukua rasilimali ya mfugaji, kuiongezea thamani kiwandani kwa kutumia stadi za vijana wetu, na hatimaye kuuza bidhaa iliyokamilika sokoni. Hii inazima kelele za wachochezi kwa kuonyesha kuwa Tanzania inaelekea katika utulivu wa kweli wa kiuchumi unaojengwa na mikono ya vijana wake wenyewe.

No comments