Nyota wa 'Pulp Fiction' akutwa nyumbani akiwa mfu




Muigizaji maarufu wa kimataifa, Peter Greene, ambaye alijipatia umaarufu kwa kuigiza nafasi za wahalifu katika filamu zilizovuma kama vile Pulp Fiction (kama 'Zed') na The Mask, amefariki dunia. Kifo chake kimezua simanzi katika tasnia ya filamu.

Peter Greene alikutwa na Polisi nyumbani kwake New York akiwa amefariki dunia. 

Polisi walifika nyumbani hapoo kuitikia wito wa simu ya dharura ya 911 iliyoripoti kwamba kuna mwanamume ambaye hakuwa anaitikia hodi nyumbani kwake kufuatia muziki kuendelea kucheza ndani ya nyumba yake kwa takribani saa 24 bila ishara yoyote ya kuzimwa.

Mpaka sasa Mamlaka bado haijatangaza sababu ya kifo chake, ingawa imesisitiza kuwa hakuna shaka ya kuwapo kwa uhalifu.

 Inasadikika alifariki Jumatano, muda mfupi baada ya kuongea na meneja wake.

Greene alikuwa amepangiwa kufanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa (siku aliyopatikana) kuondoa uvimbe usio na madhara karibu na pafu lake.

Meneja wake, Gregg Edwards, alisema walikuwa marafiki wa karibu kwa zaidi ya muongo mmoja. Alisema walizungumza kwa mara ya mwisho na Greene alisikika vizuri, ingawa alikuwa na wasiwasi kidogo kuhusu upasuaji uliokuwa umepangwa.

“Alisikika vizuri. Ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida kabisa. Alikuwa na wasiwasi kidogo kuhusu upasuaji, lakini alisema haukuwa mbaya sana,

No comments