Mabingwa wa Mitindo Kimataifa na Tanzania Watawala Jukwaa SFW 2025
Msimu wa 18 wa Swahili Fashion Week uliwakusanya zaidi ya wabunifu
50, ukiweka wazi utofauti na upekee wa mitindo ya Kiafrika na kimataifa. Jukwaa
hili lilikuwa kiunganishi cha tamaduni, kikionyesha ubunifu mkubwa kutoka kwa
wabunifu wa ndani na wa kimataifa.
Vipaji vya Ndani Vyatoka Mbali
Orodha ya wabunifu wa Kitanzania ilijumuisha majina makubwa na
vipaji vipya kutoka mikoa mbalimbali, ikithibitisha kuwa Dar es Salaam, Dodoma,
Arusha, na Morogoro ni vituo vya ubunifu.
Wabunifu hao wa Kitanzania ni: Mkwandule’son, Tory Eleganza (Dodoma), The Seamy Luxe, Jesakudo, Asili by
Naliaka, Bilan Facon, Nyuzi CAD, Thejkclothing, Neith Designs (Moshi), Jojo
African Designs (Dodoma), Miss
Kesho Fashion (Arusha), Joe Designs and Tailoring (Morogoro), Fiderine’s na
Kajo Designs.
Wengine ni Belistar Clothing Brand,
Zuh Fashion, Pwani Pure, Bella Ragazza, Kontennu, Blackcherry, Katwiga Couture,
Linea H, Faith, Men Con Styles, Michael William’s, Sam Royal Designs, Indeity,
Robes By Michelle, Shirts by Mubah, African Touch Fashion Brand, Kipenzy
Designs, Manfere Designs, Yvalia Bridal, JM International, Primus Perfect Wear,
na JV’s.
Kutoka uwanjani kimataifa walikuwepo Marion Anser (Uswisi), Dida (Italia), Kerby Young Designs (Trinidad na
Tobago), Zurika by Wambui (Kenya), Girl About (Kenya), Jodesign254 (Kenya), na
Palse (Afrika Kusini) wakiipa jukwaa sura ya dunia na mitazamo yenye tamaduni
anuwai.
Mustafa Hassanali,
Mwanzilishi na Mmiliki wa Swahili Fashion Week & Awards, alisema: “Dira
yetu daima imekuwa kuinua mitindo ya Kiafrika kufikia viwango vya kimataifa
huku tukienzi utambulisho wetu wa kipekee wa kitamaduni. Tulipoikumbatia kaulimbiu
ya Swahili Futurism, tumethibitisha imani yetu kwamba Afrika si tu chimbuko la
tamaduni bali pia ni mpaka wa uvumbuzi. Prakati ya mitindo ni ya Kiafrika jasiri,
kidijitali, na yenye mizizi imara katika ubunifu.”
Ushindani
wa Washington Benbella Emerging
Designers Competition (WBEDC) uliendelea kuibua nyota wapya, huku
mshindi, Smart Kiss,
akifuata nyayo za nyota waliowahi kung’ara kama Philista Oniang’o (Kenya,
2012). Ushiriki huu ulionyesha kwamba Swahili Fashion Week ni taa ya ubunifu na fursa kwa vipaji barani Afrika na
diaspora.
Post a Comment