KURA YAKO NI SAUTI YA MAENDELEO: Dkt. Samia Alivyobadilisha Taswira ya Miundombinu Tanzania
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, wananchi
wanahimizwa kutumia haki yao ya kidemokrasia.
Kauli ya "Kura yako ni sauti ya amani, daraja
la maendeleo, na mwanga wa kesho bora" inawahimiza Watanzania "watoke" Oktoba hii, kwenda
kupiga kura kama haki yao ya msingi.
Mfanyabiashara wa soko la Chifu Kingalu Morogoro
Yusuf Hamad Brush anasema kwamba ni vyema watu wakatoka katika majengo yao na
maeneo ya kazi kwenda kupiga kura Oktoba 29 kwa sababu hiyo ndio maana ya maendeleo.
Anasema usipoenda kupiga kura utakuwa unajimnyima
maendeleo yako mwenyewe na hasa uchaguzi wa mtu kukuwezesha kuwa na maendeleo
unayoyataka.
Anasema uchaguzi ndio njia pekee ya kupanga
maendeleo na Amani ya taifa.
Anasema yeye mwenyewe ataoenda kupiga kura kwa
kuwa anaamini kwamba kura hiyo ndio msingi wa mabadiliko anayoyataka nchini.
Katika kuhimiza upigaji kura, rekodi ya mgombea Dkt. Samia Suluhu Hassan inatumiwa
kama kielelezo cha maendeleo endelevu ya Taifa. Serikali yake imejikita katika
kubadilisha taswira ya miundombinu nchini, jambo linalochukuliwa kama msingi wa
kuendeleza uchumi na urahisi wa maisha.
Katika Sekta ya Usafiri
na Miundombinu:
Utekelezaji wa miradi mikubwa unatajwa, ikiwemo
kukamilisha ujenzi wa barabara ya juu
ya Ubungo na kuanzisha mipango ya barabara za juu mikoani. Kazi kubwa
inaendelea katika ujenzi wa reli ya
kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, hatua muhimu
itakayobadilisha usafiri nchini.
Dkt. Samia pia anatajwa kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa kama Daraja la
Kigongo–Busisi na Daraja la JPM, ambayo yanajenga daraja la maendeleo kwa
kuunganisha mikoa kwa urahisi zaidi wa kibiashara na kijamii.
Aidha, juhudi zimefanywa kuboresha viwanja vya ndege vya kisasa katika
mikoa muhimu kama Dodoma, Mwanza, na Kigoma, huku mfumo wa usafiri wa mwendokasi (DART) jijini Dar es Salaam
ukiwa umeboreshwa kwa kuongeza njia mpya na magari ya kisasa.
Mbali na miundombinu ya usafiri, Dkt. Samia pia
ametajwa kufanikisha ujenzi wa nyumba
bora za watumishi wa umma kote nchini.
Wito unaendelea kutolewa kwa wapiga kura kutumia
kura yao "kwa Samia"
mnamo Oktoba, wakisisitiza kauli mbiu ya "Kazi na utu tunasonga mbele."

Post a Comment