KAULI YA ZITTO KABWE MABADILIKO KUPITIA SANDUKU LA KURA YAUNGWA MKONO!
Na Mwandishi wetu
Kumekuwa na maoni
tofauti Mtandaoni, mengi yakiunga mkono kauli ya mmoja wa viongozi wa upinzani Zitto Kabwe ya
kuwataka watanzania kupuuza wanaotoa wito wa kutopiga kura Oktoba 29.
Katika klipu ya
moja ya hotuba zake katika kampeni akiwa Songea, Zitto anatoa wito wa wananchi
kuwafikiria wanaohimiza kutopiga kura kama watu wenye walakini ingawa wengine
anawaheshimu.
Zitto Kabwe
anayetokea ACT Wazalendo na mgombea ubunge Kigoma, alisisitiza watu
kutoka kwenda kupiga kura kwani kutofanya hivyo ni kama kununuliwa na chama
tawala kukiacha kifanye kinavyotaka.
Zitto anasema watu
wanaohimiza wengine wasishiriki katika kupiga kura wana walakini vichwani mwao
kutokana na umuhimu wa zoezi hili.
Kauli ya Zitto
inachagiza ukweli kuwa kura si tu haki, bali ni mamlaka ya kuajiri viongozi wa
nchi. Kauli ya Zitto imelenga kuwaamsha Watanzania wachanga kutokubali kupuuzia
mchakato huu.
Umuhimu wa
uchaguzi unasisitizwa kwa data za vitendo kwani taifa linatakiwa kuendelea
kusonga mbele kijamii na kiuchumi kutoka katika msingi uliowekwa.
Serikali ya sasa imewekeza mabilioni ya shilingi
katika miundombinu ya kisasa kama vile Mabasi ya Mwendokasi (BRT), ujenzi wa
Hospitali mpya 50 za wilaya, na upanuzi wa vituo vya afya.
Kwenda kupiga kura
Oktoba 29 ni fursa ya kuajiri Msimamizi: Kura inakupa wewe uwezo wa kuhoji na
kuchagua viongozi watakaoweza kulinda na kusimamia urithi huu wa Taifa, na
kuhakikisha huduma bora za afya, elimu, na usafiri zinasonga mbele.
Aidha ni fursa ya
Kudai Uwajibikaji: Vijana wanahimizwa kuhoji wagombea kwa kutumia sanduku la
kura kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakiwa miongoni mwa wanajamii.
Matusi na
uharibifu wa mali za umma (kama vile mabasi ya BRT na vizimamoto) hauna nafasi
katika siasa ya karne ya 21. Kura yako ni ya ustaarabu na ndiyo njia pekee ya
kulinda urithi wa Taifa.
Post a Comment