YANGA
imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kulazimishwa sare ya bila
kufungana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi wa
kombe la Shirikisho la soka Afrika(CAF).
Katika
mchezo wa awali Yanga ilibamizwa mabao 4-0 na USM Alger ya Algeria mchezo
uliochezwa Algeria wiki mbili zilizopita na hivyo ilihitaji sio zaidi ya
ushindi kuweka hai matumaini ya kushika moja ya nafasi mbili za juu.
Kwa upande
wa wapinzani wao Rayon hiyo ni sare yao ya pili kwenye mashindano hayo baada ya
kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Gor Mahia ya Kenya kwenye nchini Rwanda wiki
mbili zilizopita na sasa ina pointi mbili huku Yanga yenyewe ikiwa na point
moja.
Katika
mchezo wa leo Yanga ilikuwa na baadhi ya nyota wake ambao hawakucheza kwenye
mchezo uliopita dhidi ya USM Alger ambao ni beki wake mahiri Kelvin Yondani,
Obrey Chirwa , Thabani Kamusoko na Amis
Tambwe.
Lakini pia
iliendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao ni Ibrahim Ajibu na
kiungo Papy Kabamba Tshishimbi anayesumbuliwa na majeruhi.
Ikiwa na
baadhi ya nyota wake hao Yanga ilionekana kutulia kwa kiasi fulani hasa katika
sehemu ya ulinzi na kiungo ambapo uzoefu wa beki Kelvin Yondani na kiungo
Thabani Kamusoko ulionekana kuimarisha kwa kiasi fulani timu hiyo.
Rayon
walipata nafasi kadhaa za kufunga katika vipindi vyote viwili lakini
washambuliaji wake hawakuwa makini kumalizia nafasi hizo na Yanga kuonekana
kucheza vizuri zaidi katika kipindi cha pili cha mchezo huo lakini mshambuliaji
kutoka Obrey Chirwa alikosa bao la wazi kwa shuti alilopiga akiwa ndani
ya eneo la penalti kugonga mwamba.
Yanga
itakuwa mgeni wa Gor Mahia kwenye muendelezo wa mashindano hayo utakaochezwa
Nairobi, Kenya mwishoni mwa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment