RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa
kuikabidhi Simba kombe la ubingwa wa
Ligi Kuu Tanznaia Bara Jumapili Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya mchezo
dhidi ya Kagera Sugar.
Hayo yalisemwa jana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Wallace Karia na kusema pia Dk. Magufuli atakabidhiwa kombe la ubingwa wa
CECAFA na timu ya Vijana vya umri chini ya miaka 17, Serengeti boys.
“Tumemwandikia barua Rais kupitia kwa Waziri wa Habari, Sanaa Utamaiduni
na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kumwomba akubali kukabidhiwa kombe na timu
ya Vijana U-17 Serengeti boys ililotwaa mwezi uliopita nchini Burundi,” alisema
Karia
“Pia tumemwomba baada ya kukabidhiwa kombe hilo na Serengeti boys
akubali kuikabidhi Simba lao baada kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa
2017-2018 kwani ndio mchezo wa mwisho katika ligi kucheza nyumbani,” aliongeza
Karia.
Karia alisema wamemwomba Rais Dk. Magufuli apokee kombe hilo ili kuwapa
morali wachezaji hao ambao wanajiandaa na fainali za Afrika mwakani ambapo
Tanzania itakuwa mwenyeji.
Aidha alisema endapo Rais atakubali mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na
Kagera Sugar utaanza saa 8:00 mchana na kiingilio kitakuwa sh. 30000 mzunguko
ili mashabiki wengi wapate fursa ya kuingia.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais Dk Magufuli kuingia uwanja wa Taifa
akiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment