MABINGWA
wapya wa Ligi Kuu Bara Simba,jana walikabidhiwa ubingwa wao na Rais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania John Magufuri katika uwanja wa Taifa Dar es saam.
Simba
walitwaa ubingwa huo,licha ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa bao 1-0 mbele
ya Magufuri,hivyo kuvunjia rekodi yake ya kutopoteza mchezo katika Ligi hiyo.
Mshambuliaji
Edward Christopher ndiye aliyefunga bao hilo wakati mpira ukielekea ukingoni
kunako dakika ya 85,kabla ya Simba kupata penalti dakika ya 93 iliyopigwa na Emmanuel Okwi na Juma Kaseja
kupangua.
Aidha,Mgeni
rasmi wa mchezo huo,Rais Magufuri aliwapongeza Simba kwa kutwaa ubingwa huo na
kuwasihi kuendelea kupambana ikibidi watwae ubingwa wa Afrika.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi ubingwa huo,alisema Mabingwa hao walistahili kuchukua
ubingwa huo,kutokana na namna walivyopambana,lakini hakusita kuipongeza Kagera
Sugar kwa kuonesha mchezo mzuri.
Magufuri
aliipongeza Wizara husika na uwongozi wa TFF kwa kazi nzuri ambayo inaendelea
kuifanya katika kuhakikisha mpira wa Tanzania unakuwa kila siku.
Pia alizungumzia ujenzi wa uwanja mpya wa
kisasa katika Jiji la Dodoma,ambapo alisema Serikali ipo katika mchakato huo na
kuongeza matukio ya ajabu kama kung’oa viti hayapaswi kujirudia tena.
Ameziomba
Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanja na kuomba visimamiwe
kwa ubora wa hali ya juu kuhakikisha havivamiwi na mtu yoyote.
Naye,Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe, alisema uwanja wa
Taifa ndiyo utakaotumika katika michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri wa
miaka 17 itakayofanyika mwakani katika ardhi ya nyumbani.
Alisema
uwanja huo na ule wa uhuru,vinahitaji marekebisho ya hali ya juu ili kuviweka
sawa kabla ya michuano hiyo kuanza mwezi Aprili 2019.
No comments:
Post a Comment