UPEPO mbaya
umeendelea kuikumba klabu ya Yanga, baada ya leo kupoteza mchezo mwingine wa
Ligi Kuu Bara kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo
uliopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mchezo huo
unakuwa ni wa tatu mfululizo kwa timu hiyo kupoteza, ikiwa kwenye viwanja
tofauti baada ya ule wa Simba uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na
Tanzania Prisons, uliofanyika Mbeya.
Katika
mchezo huo ambao timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu, huku Mtibwa
ikijilinda zaidi kuepuka kupoteza mchezo huo.
Yanga
ilijitahidi kufanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini umakini mdogo wa
washambuliaji, Yohana Nkomola na Matheo Anthony ulifanya mchezo huo kwenda
mapumziko ukiwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha
pili kilianza kwa Mtibwa kushambulia kwa mpira mirefu ambayo hata hivyo
ilizimwa vizuri na walinzi wa pembeni, Juma Abdul na Salum Hassan.
Dakika ya
62 ilifanya mabadiliko ya kumtoa Juma
Abdul ambaye aliumia na kuingia Yusufu Suleiman, ambaye hata hivyo alionekana
kuwa na uzoefu mdogo wa Ligi.
Yanga
ilicharuka na kuanza kupeleka mashambulizi kwa kutumia mipira mirefu, ambayo
dakika ya 65 nusura wapate bao baada ya Thaban Kamusoko kugonga mwamba, kabla
ya dakika nne baadaye Matheo Anthony kufanya hivyo pia.
Mtibwa
ilionekana kudhamiria kuifunga Yanga, baada ya kufanya mabadiliko ya kumtoa
Salum Kihimbwa na kuingia Haruna Chanongo ambaye alibadilisha taswira nzima ya
mchezo huo kwa timu yake.
Wakati
mchezo ukielekea ukingoni, kiungo Thabani Kamusoko alitolewa na nafasi yake
kuchukuliwa na Festo Simon, ambapo dakika moja baadaye mchezaji Hassan Dilunga
aliipatia Mtibwa bao ambalo lilidumu hadi dakika 90 ya mchezo.
Baada ya
mchezo huo, Yanga itaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho
dhidi ya Rayon Sports utakaopigwa Mei 16 wiki hii, kwenye dimba la Taifa,Dar es
Ssalaa.
Kwa matokeo
hayo, Yanga imeendelea kushika nafasi ya tatu kwa pointi 48, ikiwa nyuma ya
Azam FC wenye pointi 52.
Yanga
katika mchezo wa kwanza wa makundi wa Kombe la Shirikisho, ilifungwa mabao 4-0
na Alger Usm ya Algeria
No comments:
Post a Comment