TIMU ya Taifa ‘Taifa Stars’ jana imeanza mazoezi kujiandaa na mashindano wachezaji
wa ndani (CHAN) yanayoandaliwa na Shirikisho la Vyama mpira barani Afrika (CAF)
Taifa stars imeingia kambini juzi kujiandaa na mchezo wao
dhidi ya Uganda utakaochezwa Uwanja wa Taifa
Julai 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kurudiwa baada ya wiki mbili jijini Kampala
Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Kocha Mkuu Kim Poulsen amesema
kuwa wachezaji wote wameingia kambini na wote wamefanya mazoezi jambo ambalo
linadhihirisha hakuna mwenye matatizo
“Wachezaji wote waliingia kambini tangu jana na leo
wamefanya mazoezi wote pia wana ari jambo linalodhihirisha mchezo dhidi ya
Uganda tutashinda” alisema Poulsen
Wachezaji wa Stars ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Aishi
Manula, Ally Mustafa, Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo,
John Bocco, Juma Liuzio na Kelvin Yondani.
Wengine ni Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Mudathiri Yahya,
Mwadini Ali, Mwinyi Kazimoto, Nadir Haroub, Salum Abubakar, Shomari Kapombe,
Simon Msuva, David Luhende na Vincent Barnabas.
No comments:
Post a Comment